ISHU YA RASHFORD BADO PASUA KICHWA

Date:

Share post:

MANCHESTER, Uingereza
KOCHA wa Manchester United, Michael Carrick, amesema bado haijafahamika kama Marcus Rashford atarudi klabuni hapo au atabaki Barcelona anakocheza kwa mkopo.

Rashford hajaitumikia Man United tangu Desemba, 2024, ikiripotiwa kuwa alikorofishana na aliyekuwa kocha wa hiyo, Ruben Amorim.

Nyota huyo alipelekwa kwa mkopo Aston Villa, kabla ya kuhamishiwa Barcelona, ambako hajaweza kujihakikishia nafasi ya kuanza kikosini.

Licha ya kuingia na kutoka katika kikosi cha kwanza, Rashford amefunga mabao 12 na kutoa ‘asisti’ 10 katika mechi 43 za mashindano mbalimbali.

Kwa mujibu wa makubaliano yao na Man United, Barcelona wanaweza kumsajili moja kwa moja endapo wataweka mezani kitita cha Pauni milioni 26.

Imeandaliwa na Hassan Mwasha

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

spot_img

Related articles

KIFO CHA BOSI KINAVYOITESA LEICESTER CITY

LONDON, UingerezaMIAKA 10 iliyopita, Leicester City waliishangaza dunia walipotwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya England (EPL) mbele ya...

BARCA YAPATA MRITHI WA LEWANDOWSKI

CATALUNYA, HispaniaKLABU ya Barcelona imeanza mipango ya kumsajili mshambuliaji wa kati wa Real Mallorca, Vedat Muriqi, ikiamini anatosha...

ARSENAL AKILI YOTE KWA MONGA

LONDON, UingerezaARSENAL ya Kaskazini mwa Jiji la London imeonesha nia ya kumsajili winga anayefanya vizuri Ligi Daraja la...

NEWCASTLE KUMUUZA MSHAMBULIAJI WA BEI MBAYA

LONDON, UingerezaKLABU ya Newcastle United itampiga bei straika raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Yoane Wissa,...