ARSENAL AKILI YOTE KWA MONGA

Date:

Share post:

LONDON, Uingereza
ARSENAL ya Kaskazini mwa Jiji la London imeonesha nia ya kumsajili winga anayefanya vizuri Ligi Daraja la Kwanza England (Championship) akiwa na Leicester City, Jeremy Monga.

Monga (16), amekuwa kwenye kiwango bora tangu alipopandishwa timu ya wakubwa ya Leicester mwishoni mwa msimu uliopita.

Nyota huyo anayecheza pia eneo la kiungo wa kati, ameingia kikosi cha kwanza mara tisa msimu huu wa Championship.

AS Roma, Bayern Munich, Atletico Madrid na Manchester United zimeripotiwa pia kuitolea macho huduma ya kinda huyo.

Hata hivyo, Leicester wametajwa kutokuwa na mpango wa kukaa mezani wala kupokea ofa ya klabu yoyote inayomtaka Monga mwishoni mwa msimu huu.

imeandaliwa na Hassan Mwasha

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

spot_img

Related articles

KIFO CHA BOSI KINAVYOITESA LEICESTER CITY

LONDON, UingerezaMIAKA 10 iliyopita, Leicester City waliishangaza dunia walipotwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya England (EPL) mbele ya...

ISHU YA RASHFORD BADO PASUA KICHWA

MANCHESTER, UingerezaKOCHA wa Manchester United, Michael Carrick, amesema bado haijafahamika kama Marcus Rashford atarudi klabuni hapo au atabaki...

BARCA YAPATA MRITHI WA LEWANDOWSKI

CATALUNYA, HispaniaKLABU ya Barcelona imeanza mipango ya kumsajili mshambuliaji wa kati wa Real Mallorca, Vedat Muriqi, ikiamini anatosha...

NEWCASTLE KUMUUZA MSHAMBULIAJI WA BEI MBAYA

LONDON, UingerezaKLABU ya Newcastle United itampiga bei straika raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Yoane Wissa,...