CATALUNYA, Hispania
KLABU ya Barcelona imeanza mipango ya kumsajili mshambuliaji wa kati wa Real Mallorca, Vedat Muriqi, ikiamini anatosha kuvaa viatu vya Robert Lewandowski.
Lewandowski raia wa Poland, anatarajiwa kuondoka Camp Nou wakati wa usajili wa dirisha kubwa, mwishoni mwa msimu huu wa 2025-26.
Awali, Barcelona walimpiga hesabu straika wa Atletico Madrid, Julian Alvarez, kabla ya kubadili ‘gia angani’ na kuhamia kwa Muriqi.
Muriqi anashika anashika nafasi ya pili katika orodha ya wafungaji msimu huu wa Ligi Kuu ya Hispania (La Liga), akiwa na mabao 21 katika mechi 30.
Kinara wa mbio hizo za kuwania kiatu cha dhahabu ni Kylian Mbappe wa Real Madrid, ambaye hata hivyo amemzidi mabao mawili pekee.
Imeandaliwa na Hassan Mwasha






