MBOWE ATOKA HOSPITALINI

Date:

Share post:

RIPOTA PANORAMA

MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe jana usiku aliruhusiwa kutoka hospitalini alikokuwa akitibiwa na kurejea nyumbani.

Mbowe alilazwa katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC baada ya kujisikia vibaya ghafla ikiwa ni saa chache kabla ya kuripoti polisi yeye na viongozi wenzake sita wa Chadema kama walivyotakiwa na polisi.

Taarifa za kitabibu zilizopatikana jana zilieleza kuwa alipofikishwa hospitali hapo alikuwa akilalamika kusumbuliwa na maumivu ya kichwa na baada ya kufanyiwa uchunguzi aligundulika kuwa anasumbuliwa na uchovu.

Akiwa hospitalini hapo aliwekewa mashine ya oksijeni kwa ajili ya kumsadia kupumua.

Afisa Uhusiano wa KCMC, Gabriel Chisseo amekaririwa akieleza kuwa Mbowe aliruhusiwa na madaktari kutoka hospitali muda wa 1:30 usiku baada ya kujiridhisha kwamba hali yake inaendelea vizuri.

Katibu wa Chadema wa Mkoa wa Kilimanjaro, Basil Lema naye alizungumzia kuimarika kwa afya ya Mbowe lakini alisema hajui alipo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

spot_img

Related articles

KIFO CHA BOSI KINAVYOITESA LEICESTER CITY

LONDON, UingerezaMIAKA 10 iliyopita, Leicester City waliishangaza dunia walipotwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya England (EPL) mbele ya...

ISHU YA RASHFORD BADO PASUA KICHWA

MANCHESTER, UingerezaKOCHA wa Manchester United, Michael Carrick, amesema bado haijafahamika kama Marcus Rashford atarudi klabuni hapo au atabaki...

BARCA YAPATA MRITHI WA LEWANDOWSKI

CATALUNYA, HispaniaKLABU ya Barcelona imeanza mipango ya kumsajili mshambuliaji wa kati wa Real Mallorca, Vedat Muriqi, ikiamini anatosha...

ARSENAL AKILI YOTE KWA MONGA

LONDON, UingerezaARSENAL ya Kaskazini mwa Jiji la London imeonesha nia ya kumsajili winga anayefanya vizuri Ligi Daraja la...