LONDON, Uingereza
UPINZANI wa Lionel Messi na Cristiano Ronaldo unaendelea, licha ya kwamba nyota hao walishaondoka katika soka la Ulaya miaka kadhaa iliyopita.
Tangu mwaka 2026 uanze, Messi amekuwa wa moto Ligi Kuu ya Marekani (MLS) akiwa na Inter Miami, kama ilivyo kwa Ronaldo anayekipiga Al Nassr ya Saudi Arabia.
Kwa mwaka huu, mwanasoka huyo wa kimataifa wa Argentina amefunga mabao tisa katika mechi 11.
Katika mabao hayo, moja alifunga kwa mkwaju wa penalti na mawili kwa mipira ya faulo iliyotinga wavuni moja kwa moja.
Wakati huo huo, Ronaldo amecheza mechi 15 tangu mwaka huu uanze, akifunga mabao 12 (matatu ya penalti) na kutoa ‘asisti’ moja.






