Wednesday, 7 October 2026

MKONGWE WA MAN UNITED ATAKA CARRICK APEWE AJIRA

MANCHESTER, Uingereza LEJENDARI wa Manchester United, Gary Pallister, amesema haoni sababu ya mabosi wa klabu hiyo kutafuta kocha wa msimu ujao wakati Michael Carrick anatosha. Hata hivyo, Pallister amesema Carrick atapaswa kupewa ajira ya moja kwa moja endapo timu hiyo itamaliza msimu huu ikiwa na tiketi ya kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao. Carrick […]

MANCHESTER, Uingereza

LEJENDARI wa Manchester United, Gary Pallister, amesema haoni sababu ya mabosi wa klabu hiyo kutafuta kocha wa msimu ujao wakati Michael Carrick anatosha.

Hata hivyo, Pallister amesema Carrick atapaswa kupewa ajira ya moja kwa moja endapo timu hiyo itamaliza msimu huu ikiwa na tiketi ya kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao.

Carrick (44), ameiwezesha Man United kufika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya England (EPL), ikitoka kupata ushindi wa bao 1-0 katika mchezo mgumu wa ugenini dhidi ya Chelsea.

Lakini, bado Man United imeendelea kuhusishwa na kocha mpya kwa ajili ya msimu ujao, huku Oliver Glasner, Andoni Iraola na Julian Nagelsmann wakitajwa zaidi kwenye kibarua hicho.

“Ni kweli hatuchezi soka la kuvutia lakini tumefanikiwa … Nafikiri (Carrick) anastahili kupewa nafasi,” amesema Pallister.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *