Wednesday, 7 October 2026

ROMERO WA SPURS KUTIMKIA ATLETICO MADRID?

MADRID, Hispania KLABU ya Atletico Madrid ya La Liga inaiwania saini ya beki wa kati wa Tottenham na timu ya Taifa ya Argentina, Cristian Romero. Nyota huyo alipata majeraha ya goti katika mechi iliyopita dhidi ya Sunderland, hivyo atamaliza msimu huu akiwa nje ya uwanja. Romero mwenye umri wa miaka 27, amecheza mechi 23 za […]

MADRID, Hispania

KLABU ya Atletico Madrid ya La Liga inaiwania saini ya beki wa kati wa Tottenham na timu ya Taifa ya Argentina, Cristian Romero.

Nyota huyo alipata majeraha ya goti katika mechi iliyopita dhidi ya Sunderland, hivyo atamaliza msimu huu akiwa nje ya uwanja.

Romero mwenye umri wa miaka 27, amecheza mechi 23 za Ligi Kuu ya England (EPL) tangu msimu huu uanze.

Tottenham wako tayari kukaa mezani na klabu inayomtaka lakini kwa sharti la kulipwa kitita cha euro milioni 65.

Real Madrid nayo imekuwa ikihusishwa na mchezaji huyo mwenye mkataba utakaokwisha mwaka 2029.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *