TATIZO LA CHELSEA LIKO HAPA TU

Date:

Share post:

LONDON, Uingereza

MKONGWE wa Chelsea, Ruud Gullit, amesema changamoto kubwa inayomtesa kocha Liam Rosenior ni timu hiyo kuwa na wachezaji wasio na ukomavu.

Kabla ya kuivaa Brighton katika mchezo wa leo Aprili 21, 2026, Blues walifungwa bao 1-0 na Manchester United.

Matokeo hayo yaliiacha katika nafasi ya sita kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya England (EPL).

Endapo mambo hayatokaa sawa, kuna hatari kubwa kwa timu hiyo kukosa tiketi ya kushiriki Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao.

Kwa mtazamo wake, Gullit amesema Chelsea ya sasa haina wachezaji wenye sifa ya uongozi ndani ya uwanja.

Mholanzi huyo ameenda mbali zaidi akisema wachezaji aina ya Luka Modric na Toni Kroos wangekuwa na mchango mkubwa kikosini.

“Najua Chelsea wanataka kushinda, lakini wamejaza makinda kikosini. Unahitaji wakongwe wa kuwafundisha hao vijana, maana kila siku wanarudia makosa yale yale,” amesema.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

spot_img

Related articles

RAIS WA TAIWAN ASITISHA ZIARA YAKE AFRIKA, CHINA IKITAJWA KUWA CHANZO

TAIPEI, TaiwanRAIS wa Taiwan, Lai Ching-te, ameahirisha ziara yake nchini Eswatini, huku akiitaja China kuwa ndiyo chanzo cha...

USIYOYAJUA KUHUSU ZIARA YA PAPA LEO BARANI AFRIKA

KIONGOZI wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Leo XIV, yuko barani Afrika kwa ziara ya siku 10 katika mataifa...

MATESO WANAYOPITIA WATOTO KATIKA MACHAFUKO YA SUDAN

DARFUR, Sudan "HALI ya watoto nchini Sudan inazidi kuwa mbaya kila baada ya saa moja." Hiyo ni kauli ya...

IRAN: TUKO TAYARI KWA VITA MAZUNGUMZO YAKISHINDIKANA

TEHRAN, IranSPIKA wa Bunge la Iran, Mohammad Bagher Ghalibaf, amesema nchi yake itakuwa tayari kwa mbinu mpya za...