LONDON, Uingereza
BEKI wa zamani wa Manchester United na timu ya Taifa ya Ufaransa, Patrice Evra, amesema Arsenal haina nafasi ya ubingwa msimu huu wa Ligi Kuu ya England (EPL).
Na badala yake, Evra ameipa nafasi hiyo Manchester City inayoshika nafasi ya pili kwenye msimamo, ikiwa imeachwa pointi tatu na Arsenal iliyoko kileleni.
Evra amedai kuwa kichapo cha mabao 2-1 walichokipata Arsenal kutoka kwa Man City wikiendi iyopita kimewatoa kwenye mbio za ubingwa.
Washika Bunduki wa Kaskazini mwa London wamebakiza mechi tano kumaliza msimu, wakati Man City wao wana sita.
“Ndiyo maana nasema siioni Arsenal (kwenye ubingwa). Siioni ikiwa na uwezo wa kuhimili presha iliyopo,” amesema.






