Wednesday, 7 October 2026

‘WASAUZI’ WAINGILIA DILI LA NWABALI KUTUA SIMBA

Na mwandishi wetu MPANGO wa Simba kumsajili kipa wa timu ya Taifa ya Nigeria ‘Super Eagles’, Stanley Nwabali, umeifikia Kaizer Chiefs na sasa klabu hiyo ya Afrika Kusini nayo inamtolea macho.​Nwabali amekuwa mchezaji asiye na klabu tangu alipoachana na Chippa United aliyojiunga nayo mwaka 2022 akitokea Katsina United.​Alionesha kiwango bora wakati wa fainali za AFCON […]

Na mwandishi wetu

MPANGO wa Simba kumsajili kipa wa timu ya Taifa ya Nigeria ‘Super Eagles’, Stanley Nwabali, umeifikia Kaizer Chiefs na sasa klabu hiyo ya Afrika Kusini nayo inamtolea macho.
​
Nwabali amekuwa mchezaji asiye na klabu tangu alipoachana na Chippa United aliyojiunga nayo mwaka 2022 akitokea Katsina United.
​
Alionesha kiwango bora wakati wa fainali za AFCON 2025 na kuzivutia klabu kadhaa kubwa, zikiwamo Al Ettifaq ya Saudi Arabia na QPR ya Ligi Daraja la Kwanza ya England (Championship).

Kwa wiki za hivi karibuni, mlinda mlango huyo amekuwa akihusishwa na soka la Tanzania, akitajwa kuwa kwenye rada za Simba.
​
Hata hivyo, sasa Wekundu wa Msimbazi watalazimika kuongeza kasi kwani mabosi wa Kaizer Chiefs nao wanamtolea macho nyota huyo wa zamani wa Enyimba.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *