BBC KUPUNGUZA WAFANYAKAZI 2,000

Date:

Share post:

LONDON, Uingereza

SHIRIKA la Utangazaji la Uingereza (BBC) limetangaza kupunguza wafanyakazi 2,000 ili kuokoa asilimia 10 ya bajeti yake ya mwaka.

BBC imeeleza kuwa asilimia 10 ya bajeti hiyo ni sawa na Dola milioni 677 kwa kipindi cha miaka miwili ijayo.

Akizungumzia hilo, Naibu Mkurugenzi Mkuu wake, Rhodri Talfan Davies, amesema, “Najua itaibua taharuki lakini tunataka kuwa wawazi juu ya changamoto iliyopo.”

Davies amesema hatua yao hiyo imetokana na mambo kadhaa, ikiwamo mfumuko wa bei, gharama za leseni, sambamba na hali mbaya ya uchumi duniani.

Mapema mwaka huu, BBC iliweka wazi kuwa inapitia changamoto za kiuchumi, ikieleza nia yake ya kupunguza asilimia 10 ya bajeti kufikia mwaka 2029.

Shirika limethibitisha kuwa utekelezaji wa mpango huo unatarajiwa kuanza rasmi Aprili Mosi, 2027.

Hatua hiyo inakuja wakati aliyekuwa Mtendaji wa Kampuni ya Google, Matt Brittin, akijiandaa kushika nafasi ya Mkurugenzi Mkuu wa BCC mapema mwezi ujao.

Imeandaliwa na Hassan Mwacha

About The Author

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

spot_img

Related articles

UCHUMI WA CHINA WAZIDI KUIMARIKA

BEIJING, China LICHA ya vita vya Marekani na Iran kuonekana kuitikisa dunia, China imeendelea kupiga hatua kubwa katika eneo...

SIKU 100 ZA RAIS MPYA WA VENEZUELA: MABADILIKO NA MASWALI MAPYA

CARACAS, Venezuela BAADA ya vikosi vya Marekani kumng’oa madarakani aliyekuwa Rais wa Venezuela, Nicolás Maduro kwenye oparesheni ya Januari...

MAELFU YA FAMILIA SUDAN BADO WAKIMBIA VITA, HALI YA MAISHA YAZIDI KUWA MBAYA

MAELFU ya familia nchini Sudan bado wanalazimika kuyakimbia makazi yao, miji na hata mipaka ya nchi kufuatia vita...

ISRAEL YAENDELEA NA OPERESHEN DHIDI YA HEZBOLLAH NCHINI LEBANON

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema Jeshi la nchi yake linaendelea na operesheni dhidi ya wanamgambo wanaoungwa...