MOURINHO KOCHA MPYA NEWCASTLE MSIMU UJAO?

Date:

Share post:

LONDON, Uingereza
UONGOZI wa Newcastle United unaangalia uwezekano wa kumrejesha Ligi Kuu ya England kocha wa zamani wa klabu za Chelsea na Manchester United, Jose Mourinho.

Kocha wa sasa, Eddie Howe, anakabiliwa na presha kubwa kutokana na mwenendo usioridhisha wa timu hiyo, licha ya usajili wa bei kubwa aliofanya.

Ukiacha jina la Mourinho anayeinoa Benfica ya Ureno, kocha mwingine anayehusishwa na Newcastle ni Roberto Mancini aliyewahi kufanya kazi Manchester City.

Wakati huu Howe akitajwa kukalia kuti kavu, Newcastle pia inatarajiwa kupoteza baadhi ya wachezaji wake muhimu mwishoni mwa msimu huu.

Miongoni mwa nyota hao ni Sandro Tonali, Tino Livramento na Anthony Gordon anayehusishwa na klabu za Bayern Munich na Arsenal.

Imeandaliwa na Hassan Mwasha

About The Author

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

spot_img

Related articles

UCHUMI WA CHINA WAZIDI KUIMARIKA

BEIJING, China LICHA ya vita vya Marekani na Iran kuonekana kuitikisa dunia, China imeendelea kupiga hatua kubwa katika eneo...

SIKU 100 ZA RAIS MPYA WA VENEZUELA: MABADILIKO NA MASWALI MAPYA

CARACAS, Venezuela BAADA ya vikosi vya Marekani kumng’oa madarakani aliyekuwa Rais wa Venezuela, Nicolás Maduro kwenye oparesheni ya Januari...

MAELFU YA FAMILIA SUDAN BADO WAKIMBIA VITA, HALI YA MAISHA YAZIDI KUWA MBAYA

MAELFU ya familia nchini Sudan bado wanalazimika kuyakimbia makazi yao, miji na hata mipaka ya nchi kufuatia vita...

ISRAEL YAENDELEA NA OPERESHEN DHIDI YA HEZBOLLAH NCHINI LEBANON

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema Jeshi la nchi yake linaendelea na operesheni dhidi ya wanamgambo wanaoungwa...