Friday, 21 August 2026

UCHUMI WA CHINA WAZIDI KUIMARIKA

BEIJING, China LICHA ya vita vya Marekani na Iran kuonekana kuitikisa dunia, China imeendelea kupiga hatua kubwa katika eneo la uchumi. Kwa mujibu wa ripoti mpya, uchumi wa Taifa hilo la Asia umekuwa mara dufu kwa kipindi kifupi cha miezi mitatu ya mwaka huu. Ripoti iliyotolewa na Serikali inaonesha kuwa Pato la Taifa limeongezeka kwa […]

BEIJING, China

LICHA ya vita vya Marekani na Iran kuonekana kuitikisa dunia, China imeendelea kupiga hatua kubwa katika eneo la uchumi.

Kwa mujibu wa ripoti mpya, uchumi wa Taifa hilo la Asia umekuwa mara dufu kwa kipindi kifupi cha miezi mitatu ya mwaka huu.

Ripoti iliyotolewa na Serikali inaonesha kuwa Pato la Taifa limeongezeka kwa asilimia tano kiwango ambacho kimetajwa kuwa kikubwa zaidi ikilinganishwa na matarajio ya awali.

Aidha, usafirishaji wa bidhaa mbalimbali, yakiwemo magari, umetajwa kuwa chanzo cha kukua haraka kwa uchumi wa nchi hiyo.

Mafanikio hao yamekuja wakati huu Marekani ikiwa imeiwekea China tozo ya asilimia 10 kwa bidhaa zake zinazoingia nchini humo.

Imeandaliwa na Hassan Mwacha

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *