MERSEYSIDE, Uingereza
KLABU ya Liverpool imeanza rasmi mbio za kunasa saini ya beki wa Bournemouth, Marcos Senesi.
Taarifa za Senesi kuondoka Bournemouth zimeongezeka tangu kocha Andoni Iraola aliposema ataondoka mwishoni mwa msimu huu.
Licha ya Bournemouth kuhaha kumbakiza, ripoti zinaeleza kuwa Senesi hana mpango wa kusaini mkataba mpya klabuni hapo.
Liverpool inahitaji mlinzi wa kati wa kusaidiana na Virgil van Dijk baada ya kupanda na kushuka kwa viwango vya Ibrahima Konate na Giovanni Leoni.
Mbali ya Liverpool, klabu zingine zilizoripotiwa kumtolea macho Senesi ni Chelsea, Manchester United, Juventus na AS Roma.
Imeandaliwa na Hassan Mwacha






