LONDON, Uingereza
NI miezi takribani miwili tu imebaki, kabla ya kuanza kwa fainali za Kombe la Dunia za mwaka huu zitakazofanyika Marekani, Canada na Mexico.
Kuelekea michuano hiyo, taarifa mbaya kwa kocha wa timu ya Taifa ya Ufaransa, Didier Deschamps, ni kutumia kwa mshambuliaji wake, Hugo Ekitike.
Ekitike Nyota huyo ameumia kifundo cha mguu akiwa na Liverpool katika michuano ya Ligi ya Mabingwa na inaelezwa kuwa majeraha hayo yatamzuia kwenda Kombe la Dunia.
Kocha wa Brazil, Carlo Ancelotti, naye ana pigo zito. Mshambuliaji wake anayekipiga Real Madrid, Rodrygo Goes, atakosekana kwenye michuano hiyo.
Goes aliumia kifundo cha mguu Machi, 2026 na kusema majeraha hayo ni makubwa zaidi kuwahi kuyapata katika maisha ya soka.
Wakati huo huo, timu ya Taifa ya Hispania imeshatangaza kumkosa mshambuliaji wake wa kati, Samu Aghehowa.
Ni pigo kwa kocha wa Hispania, Luis de la Fuente, ikizingatiwa kuwa straika huyo wa Porto alishafunga mabao 20 msimu huu.
Mabingwa watetezi, Argentina, wao watawakosa nyota wao watatu, ambao ni Valentin Carboniz Joaquin Panichelli na Juan Foyth.
Kwa upande wao, Mexico watakwenda Kombe la Dunia bila Luis Malagon na Jesus Orozco, ambao pia wanauguza majeraha yatakayowaweka nje ya uwanja na muda mrefu.
Kiungo wa zamani wa Liverpool, Takumi Minamino, naye atazikosa fainali hizo na hilo ni pigo kwa kocha wa timu ya Taifa ya Japan, Samurai Blue.
Imeandaliwa na Hassan Mwasha






