Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema Jeshi la nchi yake linaendelea na operesheni dhidi ya wanamgambo wanaoungwa mkono na Iran Hezbollah nchini Lebanon licha ya shinikizo la kimataifa kufikia makubaliano ya kusitisha mapigano.
Netanyahu amesema majeshi ya Israel yako karibu kuudhibiti mji wa kusini mwa Lebanon wa Bint Jbeil ambao anautaja kuwa ngome ya Hezbollah.
Baraza la Mawaziri la Israel linaripotiwa kukutana kujadili uwezekano wa kufikiwa makubaliano ya kusitisha mapigano lakini bado hakujatangazwa uamuzi wao kuhusiana na hilo.Iran inasisitiza kuwa Lebanon sharti ijumuishwe katika makubaliano yoyote ya kuvimaliza vita vya Mashariki ya Kati.
Imeandaliwa na Hassan Mwasha






