ARSENAL YAWAWEKA SOKONI JESUS, HAVERTZ

Date:

Share post:

LONDON, Uingereza
KATIKA kukusanya mkwanja wa kufanikisha usajili wa staa wa Atletico Madrid, Julian Alvarez, Arsenal imepanga kuwauza Gabriel Jesus na Kai Havertz.

Arsenal wanatambua mtihani mkubwa uliopo mbele yao kwani matajiri wa PSG nao wanamtolea macho Alvarez.

Alvarez, raia Argentina mwenye umri wa miaka 26, ameshafunga mabao 18 msimu huu na Atletico imesisitiza mara kadhaa kuwa mchezaji huyo hauzwi.

Hata hivyo, taarifa kutoka Hispania zimeeleza kuwa Atletico watakubali kumwachia endapo itajitokeza klabu yenye kitita cha euro milioni 120.

Kwa upande wao, Arsenal wanaamini kuwauza washambuliaji wawili, Jesus na Havertz, kutawapa fedha za kutosha kukamilisha dili hilo mwishoni mwa msimu huu.

Imeandaliwa na Hassan Mwasha

About The Author

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

spot_img

Related articles

UCHUMI WA CHINA WAZIDI KUIMARIKA

BEIJING, China LICHA ya vita vya Marekani na Iran kuonekana kuitikisa dunia, China imeendelea kupiga hatua kubwa katika eneo...

SIKU 100 ZA RAIS MPYA WA VENEZUELA: MABADILIKO NA MASWALI MAPYA

CARACAS, Venezuela BAADA ya vikosi vya Marekani kumng’oa madarakani aliyekuwa Rais wa Venezuela, Nicolás Maduro kwenye oparesheni ya Januari...

MAELFU YA FAMILIA SUDAN BADO WAKIMBIA VITA, HALI YA MAISHA YAZIDI KUWA MBAYA

MAELFU ya familia nchini Sudan bado wanalazimika kuyakimbia makazi yao, miji na hata mipaka ya nchi kufuatia vita...

ISRAEL YAENDELEA NA OPERESHEN DHIDI YA HEZBOLLAH NCHINI LEBANON

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema Jeshi la nchi yake linaendelea na operesheni dhidi ya wanamgambo wanaoungwa...