MAELFU YA FAMILIA SUDAN BADO WAKIMBIA VITA, HALI YA MAISHA YAZIDI KUWA MBAYA

Date:

Share post:

MAELFU ya familia nchini Sudan bado wanalazimika kuyakimbia makazi yao, miji na hata mipaka ya nchi kufuatia vita vilivyoanza kusambaa mwezi Aprili 2023.

Licha ya kupita kwa takribani miaka mitatu tangu kuanza kwa mzozo huo, idadi kubwa ya wananchi bado wanaishi katika hali ya kuhama hama wakitafuta usalama, huku wengi wakikosa makazi ya kudumu.

Kwa mujibu wa utafiti wa hivi karibuni uliofanywa na Baraza la Wakimbizi la Norway, uliowahusisha kaya 1,293 zilizokimbia makazi yao ndani ya Sudan na katika nchi jirani za Chad na Sudan Kusini, hali ya maisha ya waathirika inaendelea kudorora siku hadi siku.

Ripoti inaeleza kuwa familia nyingi zimejikuta katika mzunguko usioisha wa kupoteza mali zao kila wanapolazimika kuhama, hali inayozidi kufifisha matumaini ya kurejea katika maisha ya kawaida.

Takwimu zinaonyesha kuwa takribani asilimia 90 ya watu hao wamepoteza makazi yao, huku karibu robo tatu wakikosa kabisa chanzo cha kipato.

Aidha, hali ya upatikanaji wa chakula imefikia kiwango cha kutisha, ambapo zaidi ya asilimia 80 ya kaya nchini Sudan hulazimika kuruka milo mara kwa mara.

Imeandaliwa na Razaki Mkuluma

About The Author

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

spot_img

Related articles

UCHUMI WA CHINA WAZIDI KUIMARIKA

BEIJING, China LICHA ya vita vya Marekani na Iran kuonekana kuitikisa dunia, China imeendelea kupiga hatua kubwa katika eneo...

SIKU 100 ZA RAIS MPYA WA VENEZUELA: MABADILIKO NA MASWALI MAPYA

CARACAS, Venezuela BAADA ya vikosi vya Marekani kumng’oa madarakani aliyekuwa Rais wa Venezuela, Nicolás Maduro kwenye oparesheni ya Januari...

ISRAEL YAENDELEA NA OPERESHEN DHIDI YA HEZBOLLAH NCHINI LEBANON

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema Jeshi la nchi yake linaendelea na operesheni dhidi ya wanamgambo wanaoungwa...

SENESI SASA AINGIA RADA ZA LIVERPOOL

MERSEYSIDE, Uingereza KLABU ya Liverpool imeanza rasmi mbio za kunasa saini ya beki wa Bournemouth, Marcos Senesi. Taarifa za Senesi...