IRAN YAKAMATA WAPELELEZI WA ISRAEL

Date:

Share post:

TEHRAN, Iran
IMERIPOTIWA kuwa Iran inawashikilia watu wanne waliowataja kuwa ni wapelelezi wa Israel.

Taarifa hiyo inakuja wakati huu wawakilisi wa Marekani wakiangalia uwezekano wa kukaa tena mezani na Iran ili kusaka suluhu ya mgogoro unaoendelea.

Ikumbukwe, mazungumzo ya siku chache zilizopita mjini Islamabad, Pakistan, hayakuzaa matunda baada ya pande zote mbili kuondoka pasi na kufikia makubaliano.

Kumekuwapo na machafuko makubwa Mashariki ya Kati tangu vikosi vya kijeshi vya Marekani na Israel vilipoungana kuishambulia Iran wiki sita zilizopita.

Juu ya kukamatwa kwa watu wanne hao, Shirika la Habari la Iran, IRNA, limedai kuwa wameshakabidhiwa kwa mamlaka ili hatua zaidi ziweze kuchukuliwa.

“Wanaoshikiliwa wamekuwa wakiipatia Mossad (Shirika la ujasusi la Israel) picha za maeneo nyeti ya kambi za kijeshi (za Iran) kupitia mitandao,” imeeleza taarifa ya IRNA.

Imeandaliwa na Hassan Mwasha

About The Author

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

spot_img

Related articles

UCHUMI WA CHINA WAZIDI KUIMARIKA

BEIJING, China LICHA ya vita vya Marekani na Iran kuonekana kuitikisa dunia, China imeendelea kupiga hatua kubwa katika eneo...

SIKU 100 ZA RAIS MPYA WA VENEZUELA: MABADILIKO NA MASWALI MAPYA

CARACAS, Venezuela BAADA ya vikosi vya Marekani kumng’oa madarakani aliyekuwa Rais wa Venezuela, Nicolás Maduro kwenye oparesheni ya Januari...

MAELFU YA FAMILIA SUDAN BADO WAKIMBIA VITA, HALI YA MAISHA YAZIDI KUWA MBAYA

MAELFU ya familia nchini Sudan bado wanalazimika kuyakimbia makazi yao, miji na hata mipaka ya nchi kufuatia vita...

ISRAEL YAENDELEA NA OPERESHEN DHIDI YA HEZBOLLAH NCHINI LEBANON

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema Jeshi la nchi yake linaendelea na operesheni dhidi ya wanamgambo wanaoungwa...