DANGOTE, TRUMP WATAJWA WATU WENYE USHAWISHI ZAIDI DUNIANI

Date:

Share post:

WASHINGTON DC, Marekani
MFANYABIASHARA maarufu Afrika, Aliko Dangote, ni miongoni mwa watu 100 wenye ushawishi duniani, kwa mujibu wa ripoti ya mwaka 2026 ya Jarida la TIME.

Mbali ya bilionea huyo raia wa Nigeria, wengine walioingia kwenye orodha ya watu 100 wenye ushawishi ni Rais wa Marekani, Donald Trump, Xi Jinping wa China, na Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu.

Wengine ni Waziri Mkuu wa Canada, Mark Carney, na Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Leo XIV.

Kwa Dangote, hii inakuwa mara yake ya pili kutambuliwa na TIME kama miongoni mwa watu 100 wenye ushawishi duniani.

Ikumbukwe, tajiri huyo aliingia kwa mara ya kwanza katika ripoti yao ya mwaka 2014 kwa mchango mkubwa alionao kwenye sekta ya biashara.

Dangote anafahamika kwa uwekezaji wake mkubwa katika uchakataji wa bidhaa za chakula, kilimo, miundombinu na nishati.

Pia, kupitia Taasisi yake ya Aliko Dangote, amekuwa akitumia fedha zake kusaidia sekta za afya, elimu na kuyawezesha kiuchumi makundi mbalimbali katika jamii.

Imeandaliwa na Hassan Mwasha

About The Author

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

spot_img

Related articles

UCHUMI WA CHINA WAZIDI KUIMARIKA

BEIJING, China LICHA ya vita vya Marekani na Iran kuonekana kuitikisa dunia, China imeendelea kupiga hatua kubwa katika eneo...

SIKU 100 ZA RAIS MPYA WA VENEZUELA: MABADILIKO NA MASWALI MAPYA

CARACAS, Venezuela BAADA ya vikosi vya Marekani kumng’oa madarakani aliyekuwa Rais wa Venezuela, Nicolás Maduro kwenye oparesheni ya Januari...

MAELFU YA FAMILIA SUDAN BADO WAKIMBIA VITA, HALI YA MAISHA YAZIDI KUWA MBAYA

MAELFU ya familia nchini Sudan bado wanalazimika kuyakimbia makazi yao, miji na hata mipaka ya nchi kufuatia vita...

ISRAEL YAENDELEA NA OPERESHEN DHIDI YA HEZBOLLAH NCHINI LEBANON

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema Jeshi la nchi yake linaendelea na operesheni dhidi ya wanamgambo wanaoungwa...