WAZIRI WA ZAMANI AFUTIWA MASHITAKA YA UGAIDI

Date:

Share post:

LAGOS, Nigeria
MAMLAKA nchini Nigeria zimemfutia kesi ya kufadhili vikundi vya kigaidi iliyokuwa ikimkabili Waziri wa Sheria wa zamani, Abubakar Malami.

Malami alifunguliwa mashitaka mwanzoni mwa mwaka huu, akitajwa kuvipa msaada wa fedha vikundi hivyo vya kigaidi.

Msingi wa mashitaka hayo, kwa mujibu wa mamlaka, ulitokana na kitendo cha Waziri huyo kutowashitaki wafadhili wa ugaidi, licha ya majina yao kufikishwa ofisini kwake.

Sasa, kwa mujibu wa mwanasheria wake, Adedayo Adedeji, Malami ameondoshewa mashitaka hayo na kubaki na yake ya kumiliki silaha aina ya bastola bila leseni.

Mashitaka hayo yanamuhusu pia mtoto wake wa kiume, licha ya wote wawili kukana mahakamani.

Imeandaliwa na Hassan Mwasha

About The Author

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

spot_img

Related articles

UCHUMI WA CHINA WAZIDI KUIMARIKA

BEIJING, China LICHA ya vita vya Marekani na Iran kuonekana kuitikisa dunia, China imeendelea kupiga hatua kubwa katika eneo...

SIKU 100 ZA RAIS MPYA WA VENEZUELA: MABADILIKO NA MASWALI MAPYA

CARACAS, Venezuela BAADA ya vikosi vya Marekani kumng’oa madarakani aliyekuwa Rais wa Venezuela, Nicolás Maduro kwenye oparesheni ya Januari...

MAELFU YA FAMILIA SUDAN BADO WAKIMBIA VITA, HALI YA MAISHA YAZIDI KUWA MBAYA

MAELFU ya familia nchini Sudan bado wanalazimika kuyakimbia makazi yao, miji na hata mipaka ya nchi kufuatia vita...

ISRAEL YAENDELEA NA OPERESHEN DHIDI YA HEZBOLLAH NCHINI LEBANON

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema Jeshi la nchi yake linaendelea na operesheni dhidi ya wanamgambo wanaoungwa...