MKUU WA MKOA WA LINDI AKAGUA MIRADI YA MWENGE WA UHURU 2026

Date:

Share post:

Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Mhe. Zainab Telack, ameongoza Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa kufanya ziara ya kukagua miradi inayotarajiwa kutembelewa na Mwenge wa Uhuru mwaka 2026.

Ziara hiyo imefanyika leo Aprili 16, 2026, ikiwa na lengo la kuhakikisha miradi yote iko katika hali nzuri na tayari kwa mapokezi ya Mwenge wa Uhuru utakaopita mkoani humo.

Akizungumza wakati wa ukaguzi huo, Mhe. Telack amesisitiza umuhimu wa maandalizi ya kina ili kuhakikisha miradi hiyo inaleta tija kwa wananchi na kuendana na malengo ya maendeleo ya serikali.

Kamati hiyo imepanga kufanya ukaguzi katika halmashauri zote za Mkoa wa Lindi ili kujiridhisha na utekelezaji wa miradi hiyo.

Kwa mujibu wa ratiba, Mwenge wa Uhuru unatarajiwa kuingia mkoani Lindi Aprili 27, 2026 kupitia Halmashauri ya Kilwa, ukitokea Halmashauri ya Ruangwa ambako maandalizi ya mapokezi yanaendelea.

About The Author

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

spot_img

Related articles

UCHUMI WA CHINA WAZIDI KUIMARIKA

BEIJING, China LICHA ya vita vya Marekani na Iran kuonekana kuitikisa dunia, China imeendelea kupiga hatua kubwa katika eneo...

SIKU 100 ZA RAIS MPYA WA VENEZUELA: MABADILIKO NA MASWALI MAPYA

CARACAS, Venezuela BAADA ya vikosi vya Marekani kumng’oa madarakani aliyekuwa Rais wa Venezuela, Nicolás Maduro kwenye oparesheni ya Januari...

MAELFU YA FAMILIA SUDAN BADO WAKIMBIA VITA, HALI YA MAISHA YAZIDI KUWA MBAYA

MAELFU ya familia nchini Sudan bado wanalazimika kuyakimbia makazi yao, miji na hata mipaka ya nchi kufuatia vita...

ISRAEL YAENDELEA NA OPERESHEN DHIDI YA HEZBOLLAH NCHINI LEBANON

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema Jeshi la nchi yake linaendelea na operesheni dhidi ya wanamgambo wanaoungwa...