LONDON, Uingereza
KUFIKIA hatua hii, ambapo Bayern Munich, Arsenal, Atletico Madrid na PSG ndizo zilizoingia nusu fainali, kuna vita ya pasi za mabao (asisti) inayoendelea.
Staa wa Bayern Munich, Michael Olise, na mwenzake wa Real Madrid, Vinicius Junior, ndiyo wanaoongoza, kila mmoja akiwa na ‘asisti’ tisa.
Wanaofuata ni Pierre-Emerick Aubameyang (Marseille), Antoine Griezmann (Atletico), Achraf Hakimi (PSG) na Khvicha Kvaratskhelia (PSG), kila mmoja akiwa na tano.
Hivyo, kwa kuwa Madrid na Marseille zimeshaondoshwa kwenye michuano hiyo, vita imebaki kwa Olise, Griezmann, Hakimi na Kvaratskhelia.
Je, nani atamaliza msimu huu wa Ligi ya Mabingwa akiwa mfalme wa asisti? Ni suala la kusubiri na kuona.
Imeandaliwa na Hassan Mwasha






