LONDON, Uingereza
LICHA ya Real Madrid kusukumwa nje ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, mshambuliaji wake raia wa Ufaransa, Kylia Mbappe, ndiye anayeongozwa kwa kupachika mabao msimu huu wa michuano hiyo.
Mbappe anaongoza akiwa ameshazifumania nyavu mara 15, akimzidi matatu tu straika wa Bayern Munich raia wa England, Harry Kane.
Tofauti na Mbappe, Kane bado anaendelea na mashindano na timu yake itaivaa PSG katika hatua inayofuata ya nusu fainali.
Anayeshika nafasi ya tatu kwenye orodha ya wafungaji ni mshambuliaji wa Newcastle United, Anthony Gordon, mwenye mabao 10.
Nyuma yake, anafukuziwa na wakali watatu; Julian Alvarez (9), Erling Haaland na Khvicha Kvaratskhelia (8).
Imeandaliwa na Hasaan Mwasha






