KIPCHOGE ASIKITIKA TOTTENHAM KUKARIBIA KUSHUKA DARAJA

Date:

Share post:

CAPE TOWN, Afrika Kusini

MWANARIADHA wa mbio ndefu raia wa Kenya, Eliud Kipchoge, ameeleza kuumizwa kwake na kitendo cha Tottenham kuwa hatarini kushuka daraja msimu huu wa Ligi Kuu ya England (EPL).

Klabu hiyo ya Kaskazini mwa London iko kwenye wakati mgumu, ikishika nafasi ya 18 kwenye msimamo wa Ligi hiyo ya timu 20.

Kipchoge amekuwa shabiki wa Tottenham kwa miaka mingi, ikikumbukwa kuwa aliwahi kutembelea makao makuu ya klabu hiyo mara mbili (2018 na 2019).

Itakumbukwa kuwa alifanya ziara hiyo wakati huo Mkenya mwenzake, Victor Wanyama, akiwa mchezaji wa Tottenham.

“Mimi bado ni shabiki wa Tottenham. Tunapitia kipindi kigumu. Tuko kati ya timu tatu zilizo kwenye mstari wa kushuka daraja. Sijui kama tutanusurika,” amesema.

Imeandaliwa na Hassan Mwasha

About The Author

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

spot_img

Related articles

UCHUMI WA CHINA WAZIDI KUIMARIKA

BEIJING, China LICHA ya vita vya Marekani na Iran kuonekana kuitikisa dunia, China imeendelea kupiga hatua kubwa katika eneo...

SIKU 100 ZA RAIS MPYA WA VENEZUELA: MABADILIKO NA MASWALI MAPYA

CARACAS, Venezuela BAADA ya vikosi vya Marekani kumng’oa madarakani aliyekuwa Rais wa Venezuela, Nicolás Maduro kwenye oparesheni ya Januari...

MAELFU YA FAMILIA SUDAN BADO WAKIMBIA VITA, HALI YA MAISHA YAZIDI KUWA MBAYA

MAELFU ya familia nchini Sudan bado wanalazimika kuyakimbia makazi yao, miji na hata mipaka ya nchi kufuatia vita...

ISRAEL YAENDELEA NA OPERESHEN DHIDI YA HEZBOLLAH NCHINI LEBANON

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema Jeshi la nchi yake linaendelea na operesheni dhidi ya wanamgambo wanaoungwa...