DODOMA WAMUAGA HAYATI RAIS DK. MAGUFULI

Date:

Share post:

 

Msafara wa magari wenye mwili wa Hayati Rais Dk. John Magufuli ukiingia Uwanja wa Jamhuri kwa ajili ya mazishi ya kitaifa.

NA RIPOTA WA PANORAMA

HAYATI Rais Dk. John Pombe Magufuli, aliyefariki dunia Machi 17, 2021 katika Hospitali ya Mzena jijini Dar es Salaam, leo ameagwa na wananchi wa Mkoa wa Dodoma na mikoa ya jirani katika Uwanja wa Jamhuri.

Wananchi wa Dodoma na mikoa ya jirani wamepata nafasi na kumuaga Hayati Rais Dk. Magufuli katika mazishi ya kitaifa yaliyoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan na kuhudhuriwa na marais na wakuu wa nchi 17, viongozi wa mashirika ya kimataifa, marais wastaafu wa Tanzania, Ali Hassan Mwinyi na Dk. Jakaya Mrisho Kikwete pamoja na viongozi wa kitaifa.

Mwili wa Hayati Rais Dk. Magufuli umewafikishwa  katika Uwanja wa Jamhuri Dodoma majira ya saa nne na dakika arobaini asubuhi lakini wananchi wa Dodoma na mikoa ya jirani walianza kufika uwanja hapo mapema asubuhi 


Janeth Magufuli, mjane wa Hayati Rais Dk. John Pombe Magufuli akiwa ameghubikwa na huzuni wakati wa mazishi ya kitaifa ya mumewe.

 

Mazishi hayo ya kitaifa yalitanguliwa na sala kabla ya Rais Samia, Janeth Magufli (mjane ya Hayati Rais Dk. Magufuli) marais na viongozi wa mataifa mbalimbali ya Afrika kutoa heshima za mwisho mbele ya jeneza lililokuwa na mwili wake.

Baada ya shughuli hiyo, gari maalumu la kijeshi lililokuwa na mwili wake lilizunguka mara tano katika Uwanja wa Jamhuri kwa ajili ya kuwapa wananchi fursa ya kumuaga na baada ya hapo, mwili huo ulipitishwa katika mitaa maarufu ya Jiji la Dodoma iliyokuwa imefurika maelfu ya wananchi waliokuwa wamejipanga kutoa heshima zao za mwisho.

Gari maalumu la kijeshi lililokuwa na mwili wa Hayati Rais Dk. Magufuli lilipita katika mzunguko wa barabara za Bahi na Shule ya Msingi Uhuru, Barabara ya Iringa, Mirembe Hospitali, Barabara ya Kigamboni, mzunguko wa Jamatini, Bunge, Emmaus ya Pili mpaka mataa, Barabara ya Mataa kuelekea makazi ya Waziri Mkuu, African Dream kuelekea njia panda ya wajenzi hadi uwanja wa ndege.


 

Wananchi wa Dodoma wakiwa wamejipanga barabarani kuuaga mwili wa Hayati Rais Dk. Johm Pombe Magufuli.


 Wananchi wa Dodoma wakiwa katika Uwanja wa Jamhuri wakati wa mazishi ya kitaifa ya Hayati Rais Dk. John Pombe Magufuli

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

spot_img

Related articles

SOMA HIYO! ISRAEL NDIYO WAASISI WA MIKWAJU YA PENALTI

LONDON, Uingereza NI jioni ya Agosti 5, 1970 kwenye Uwanja wa Boothferry Park mjini Hull, Manchester United ikiwa ugenini...

AMEJIPATA! LAMPARD ALIVYOREJEA EPL AKIWEKA REKODI

LONDON, Uingereza IKIWA ni miezi 18 tu imepita tangu alipoajiriwa, Frank Lampard ameiwezesha Coventry City kupanda daraja na kurejea...

USICHUKULIE POA! PATORANKING ALIUZA SUMU YA PANYA MITAANI KABLA YA ‘KUTOBOA’

LAGOS, Nigeria WAHENGA walisema maisha ni safari yenye milima na mabonde. Kwamba katika kuishi kwako, si nyakati zote zitakuwa...

KIFO CHA BOSI KINAVYOITESA LEICESTER CITY

LONDON, UingerezaMIAKA 10 iliyopita, Leicester City waliishangaza dunia walipotwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya England (EPL) mbele ya...