AMEJIPATA! LAMPARD ALIVYOREJEA EPL AKIWEKA REKODI

Date:

Share post:

LONDON, Uingereza

IKIWA ni miezi 18 tu imepita tangu alipoajiriwa, Frank Lampard ameiwezesha Coventry City kupanda daraja na kurejea Ligi Kuu ya England (EPL).

Lampard aliyewahi kucheza na kuinoa Chelsea, anakuwa kocha pekee kuirudisha EPL tangu Coventry iliposhuka miaka 25 iliyopita.

Timu hiyo imekata tiketi ya kucheza EPL msimu ujao (2026-27) baada ya sare ya bao 1-1 dhidi ya Blackburn, huku wakiwa na mechi tatu mkononi.

ANGUKO LAKE EPL

Aliwahi kuinoa Everton kwa miezi 12 lakini aliishia kufukuzwa kutokana na mwenendo mbaya wa timu hiyo kwenye Ligi.

Hata alipokabidhiwa Chelsea, bado hali ilikuwa mbaya kwa upande wake. Alitimuliwa akiwa ameshinda mechi moja tu kati ya 11 alizokaa kwenye benchi la ufundi.

HAIKUWA RAHISI

Coventry ilimpa ajira miezi 18 iliyopita, akichukua nafasi ya kocha Mark Robins aliyekuwa ameitoa timu hiyo League Two (Daraja la Pili) hadi Championship (Daraja la Kwanza).

Aliikuta timu hiyo ikiwa nafasi ya 17 kwenye msimamo wa Championship na msimu wa 2024-25 uliisha wakiwa wameshindwa kupanda Daraja baada ya kufungwa na Sunderland katika nusu fainali ya Sunderland.

Wakati wa dirisha kubwa, Lampard alifanya usajili wa kuboresha kikosi kwa kuwanasa Kaine Kesler-Hayden (Aston Villa), Luke Woolfenden (Ipswich) na Carl Rushworth (Brighton).

Wakati huo pia, alifanikiwa kuwabakiza wachezaji muhimu, wakiwamo Bobby Thomas na Milan van Ewijk aliyekuwa kwenye rada za Wolfsburg ya Bundesliga.

Chini ya Lampard, mshambuliaji Jack Rudoni amekuwa moto wa kuotea mbali, akifunga mabao 15 katika mechi 17 alizocheza akiwa na kocha huyo.

Ni kutokana na mikakati mizuri kwenye usajili, sambamba na mbinu zake uwanjani, Coventry imeshinda mechi 42 kati ya 79 ilizocheza chini ya Lampard aliyeajiriwa Novemba, 2024.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

spot_img

Related articles

SOMA HIYO! ISRAEL NDIYO WAASISI WA MIKWAJU YA PENALTI

LONDON, Uingereza NI jioni ya Agosti 5, 1970 kwenye Uwanja wa Boothferry Park mjini Hull, Manchester United ikiwa ugenini...

USICHUKULIE POA! PATORANKING ALIUZA SUMU YA PANYA MITAANI KABLA YA ‘KUTOBOA’

LAGOS, Nigeria WAHENGA walisema maisha ni safari yenye milima na mabonde. Kwamba katika kuishi kwako, si nyakati zote zitakuwa...

KIFO CHA BOSI KINAVYOITESA LEICESTER CITY

LONDON, UingerezaMIAKA 10 iliyopita, Leicester City waliishangaza dunia walipotwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya England (EPL) mbele ya...

ISHU YA RASHFORD BADO PASUA KICHWA

MANCHESTER, UingerezaKOCHA wa Manchester United, Michael Carrick, amesema bado haijafahamika kama Marcus Rashford atarudi klabuni hapo au atabaki...