MWANAFUNZI AFARIKI AKICHEZA MPIRA

Date:

Share post:

TANGA

MWANAFUNZI wa kidato cha nne wa Shule ya Sekondari Chief Mang’enya iliyopo Wilaya ya Muheza, mkoani Tanga, Abdallah Msenga amefariki dunia baada ya kugongana kichwa na mwanafunzi mwanzeke, Abdallah Bakari.

Tukio hilo limetokea wakati wa mechi ya ligi ya ndani ya shule hiyo iliyokuwa ikizikutanisha timu za wanafunzi wa kidato cha nne mkondo wa AB na CB.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Almanus Muchunguzi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema limetoa Februari 22, 2026 katika viwanja vya shule hiyo.

Kamanda Muchunguzi amesema mwanafunzi huyo alikuwa akigombea mpira na mchezaji mwenzake wa timu pinzani, Abdallah Bakari ndipo walipogongana vichwa na kusababisha marehemu kuanguka chini.

“Waligongana na marehemu aligongwa sehemu ya kushoto na kukimbizwa katika hospitali teule ya Wilaya ya Muheza ingawa alipoteza maisha wakati akipatiwa matibabu,”  amesema Kamanda Muchunguzi,

About The Author

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

spot_img

Related articles

BBC KUPUNGUZA WAFANYAKAZI 2,000

LONDON, Uingereza SHIRIKA la Utangazaji la Uingereza (BBC) limetangaza kupunguza wafanyakazi 2,000 ili kuokoa asilimia 10 ya bajeti yake...

MATUMAINI YAKONEKANA BAADA YA MAREKANI NA IRAN KUPATANISWA NA PAKISTAN

Maafisa wa Pakistan wanatarajia kupatikana kwa “mafaanikio makubwa” katika mazungumzo yanayoendelea kati ya Iran na Marekani kuhusu mpango...

IRAN YAKAMATA WAPELELEZI WA ISRAEL

TEHRAN, IranIMERIPOTIWA kuwa Iran inawashikilia watu wanne waliowataja kuwa ni wapelelezi wa Israel. Taarifa hiyo inakuja wakati huu wawakilisi...

DANGOTE, TRUMP WATAJWA WATU WENYE USHAWISHI ZAIDI DUNIANI

WASHINGTON DC, MarekaniMFANYABIASHARA maarufu Afrika, Aliko Dangote, ni miongoni mwa watu 100 wenye ushawishi duniani, kwa mujibu wa...