RAFIKI AMCHIMBIA MKWARA LIONEL MESSI

Date:

Share post:

MIAMI, Marekani
KOCHA mpya wa Inter Miami, Guillermo Hoyos, amesema urafiki wake na Lionel Messi haumaanishi kuwa atamlegezea mazoezini.

Hoyos mwenye umri wa miaka 62, amekabidhiwa mikoba ya kuinoa Inter Miami anayocheza mshambuliaji huyo.

Urafiki wake na Messi ulianzia wakati Hoyos akiwa Barcelona, Messi akicheza timu za vijana klabuni hapo.

Kabla ya kupewa mikoba ya ukocha iliyoachwa na Javier Mascherano aliyejiuzulu hivi karibuni, aliwahi kuwa Mkurugenzi wa Michezo wa Inter Miami.

Akizungumza baada ya kuajiriwa katika nafasi ya ukocha, amesema: “Urafiki haupingiki. Tuna urafiki wa miaka mingi.

“Hata hivyo, urafiki wetu haumaanishi kuwa nitalegeza baadhi ya misimamo yangu kama kocha kwa kumtazama usoni kila siku.”

Imeandaliwa na Hassan Mwasha

About The Author

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

spot_img

Related articles

UCHUMI WA CHINA WAZIDI KUIMARIKA

BEIJING, China LICHA ya vita vya Marekani na Iran kuonekana kuitikisa dunia, China imeendelea kupiga hatua kubwa katika eneo...

SIKU 100 ZA RAIS MPYA WA VENEZUELA: MABADILIKO NA MASWALI MAPYA

CARACAS, Venezuela BAADA ya vikosi vya Marekani kumng’oa madarakani aliyekuwa Rais wa Venezuela, Nicolás Maduro kwenye oparesheni ya Januari...

MAELFU YA FAMILIA SUDAN BADO WAKIMBIA VITA, HALI YA MAISHA YAZIDI KUWA MBAYA

MAELFU ya familia nchini Sudan bado wanalazimika kuyakimbia makazi yao, miji na hata mipaka ya nchi kufuatia vita...

ISRAEL YAENDELEA NA OPERESHEN DHIDI YA HEZBOLLAH NCHINI LEBANON

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema Jeshi la nchi yake linaendelea na operesheni dhidi ya wanamgambo wanaoungwa...