RAIS SAMIA AZINDUA JENGO LA ULINZI WA TAIFA

Date:

Share post:

DODOMA:

RAIS na Amiri Jeshi Mkuu, Dk. Samia Suluhu Hassan, amesema jengo jipya la Makao Makuu ya Ulinzi wa Taifa jijini Dodoma ni alama ya ukomavu wa taifa na uthibitisho wa uwezo wa watanzania kupanga, kuamua na kutekeleza miradi mikubwa kwa kutumia rasilimali na wataalamu wa ndani.

Akizungumza Februari 24, 2026 katika uzinduzi wa jengo hilo uliofanyika jijini Dodoma, Rais Samia amesema uwekezaji huo unaimarisha uhuru wa maamuzi ya taifa na kulipa heshima katika masuala ya ulinzi akibainisha kuwa Tanzania sasa ni miongoni mwa nchi zilizotoa kipaumbele cha juu katika shughuli za ulinzi.

Hata hivyo, ameonya kuwa majengo hayo yasibaki kuwa fahari ya muonekano pekee, bali yatumike kikamilifu kuimarisha usimamizi wa ulinzi wa taifa.

Alisisitiza kuwa makao makuu hayo yanapaswa kuwa kituo cha fikra, uchambuzi wa kitaalamu na uratibu wa kisayansi wa mikakati ya ulinzi inayoendana na mabadiliko ya wakati.

Rais Samia ameeleza kuwa katika mazingira ya sasa ya usalama wa dunia, ulinzi hauhusiani na silaha pekee bali unategemea pia upatikanaji na uchambuzi wa taarifa, matumizi ya teknolojia za kisasa, mifumo madhubuti ya mawasiliano pamoja na ubobezi wa hali ya juu wa kitaalamu.

Amebainisha kuwa baada ya kulitembelea jengo hilo ameridhishwa na hatua zilizofikiwa katika kuzingatia matumizi ya teknolojia na mifumo ya kisasa huku akisisitiza umuhimu wa kuongeza nguvu katika awamu zijazo za ujenzi.

Rais Samia ameahidi kuhakikisha kuwa awamu zilizobaki za mradi huo zinakamilishwa kwa wakati ili kuendelea kuimarisha uwezo wa taifa katika kulinda mipaka, maslahi na usalama wa nchi

About The Author

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

spot_img

Related articles

UCHUMI WA CHINA WAZIDI KUIMARIKA

BEIJING, China LICHA ya vita vya Marekani na Iran kuonekana kuitikisa dunia, China imeendelea kupiga hatua kubwa katika eneo...

SIKU 100 ZA RAIS MPYA WA VENEZUELA: MABADILIKO NA MASWALI MAPYA

CARACAS, Venezuela BAADA ya vikosi vya Marekani kumng’oa madarakani aliyekuwa Rais wa Venezuela, Nicolás Maduro kwenye oparesheni ya Januari...

MAELFU YA FAMILIA SUDAN BADO WAKIMBIA VITA, HALI YA MAISHA YAZIDI KUWA MBAYA

MAELFU ya familia nchini Sudan bado wanalazimika kuyakimbia makazi yao, miji na hata mipaka ya nchi kufuatia vita...

ISRAEL YAENDELEA NA OPERESHEN DHIDI YA HEZBOLLAH NCHINI LEBANON

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema Jeshi la nchi yake linaendelea na operesheni dhidi ya wanamgambo wanaoungwa...