TUME YA UCHUNGUZI YAKUTANA NA OLE SABAYA

Date:

Share post:

DAR ES SALAAM: 

TUME ya kuchunguza matukio ya uvunjifu wa amani yaliyojitokeza wakati na baada ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 29, Februari 24 imekutana na aliyewahi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya.

Mahojiano hayo ya tume na Sabaya yamefanyika katika ofisi za tume hiyo zilizopo Benki Kuu ya Tanzania (BoT) mkoani hapa, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kukusanya taarifa, maoni na ushauri kutoka kwa watu mbalimbali wakiwemo viongozi wa sasa na wastaafu.

Imeelezwa kuwa tume na Sabaya walijadili kwa kina namna matukio ya uvunjifu wa amani yalivyoanza, athari zake kwa wananchi, mali zao na miundombinu pamoja na ushauri na mapendekezo ya namna ya kudhibiti na kuzuia matukio kama hayo yasijirudie siku zijazo.

Hivi karibuni mamlaka ya uteuzi imeiongezea tume muda wa siku arobaini na mbili (42) kuanzia Februari 20, 2026 ili iweze kukamilisha uchunguzi wa matukio ya uvunjifu wa amani ya wakati na baada ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 29, 2025 na kuitaka ikamilishe kazi na kuwasilisha taarifa yake kabla au ifikapo Aprili 3, 2026.

Kwa sasa tume inaendelea na mahojiano na waathirika wa matukio hayo kwa ajili ya hatua zaidi kama taifa ili matukio kama hayo yasijirudie tena

About The Author

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

spot_img

Related articles

UCHUMI WA CHINA WAZIDI KUIMARIKA

BEIJING, China LICHA ya vita vya Marekani na Iran kuonekana kuitikisa dunia, China imeendelea kupiga hatua kubwa katika eneo...

SIKU 100 ZA RAIS MPYA WA VENEZUELA: MABADILIKO NA MASWALI MAPYA

CARACAS, Venezuela BAADA ya vikosi vya Marekani kumng’oa madarakani aliyekuwa Rais wa Venezuela, Nicolás Maduro kwenye oparesheni ya Januari...

MAELFU YA FAMILIA SUDAN BADO WAKIMBIA VITA, HALI YA MAISHA YAZIDI KUWA MBAYA

MAELFU ya familia nchini Sudan bado wanalazimika kuyakimbia makazi yao, miji na hata mipaka ya nchi kufuatia vita...

ISRAEL YAENDELEA NA OPERESHEN DHIDI YA HEZBOLLAH NCHINI LEBANON

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema Jeshi la nchi yake linaendelea na operesheni dhidi ya wanamgambo wanaoungwa...