MFUMO WA KUMBUKUMBU KUPUNGUZA MALALAMIKKO TASAF

Date:

Share post:

 

Afisa anayeshughulikia malalamiko wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii, (TASAF) Makwinja Damas Yusuph akizungumza katika mafunzo ya kuwejengea uwezo watendaji wa mfuko huo, yaliyofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Jiji la Tanga

MASHAKA MHANDO, TANGA

MATUMIZI ya mfumo wa kuweka kumbukumbu, utasaidia kupunguza malalamiko ya wanufaika wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini kupitia mradi unaotekelezwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF).

Akizungumza katika mafunzo ya kuwajengea uwezo watendaji wa TASAF, kutoka halmashauri 35 za mikoa ya Tanga, Morogoro, Kilimanjaro, Arusha na Pemba, ofisa anayeshughulikia malalamiko wa mfuko huo, Makwinja Dismas Yusuph alisema mfumo huo utapunguza malalamiko kwa kiasi kikubwa. 

“Madhumuni ya mafunzo haya kwa watendaji wetu kutoka halmashauri za wilaya na majiji 35, utasaidia kupunguza malalamiko ambayo mara nyingi yamekuwa yakitolewa na walengwa wa mpango wa kunusuru kaya masikini,” alisema Makwinja. 

Alisema mpango wa kunusuru kaya masikini wamekuwa wakitoa ruzuku kwa kaya zinazostahili kwa kukidhi vigezo vya elimu, afya na lishe. 

Watendaji wa TASAF wakiwa katika mafunzo ya kujengewa uwezo yaliyofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Jiji la Tanga


“Sasa unapokuwa na mradi kama huu (Social Protection)  lazima unazalisha malalamiko mengi kwa sababu unagusa jamii moja kwa moja na malalamiko ni mengi, ” alisema. 

Ofisa huyo alisema kufuatia hali hiyo mpango umeweka kitengo maalum (Call Center) chenye wataalamu waliobobea katika fani mbalimbali utakaoshughulikia malalamiko yatakayotolewa. 

Alisema kitengo hicho kitapokea simu za malalamiko, itayachunguza kama yana ukweli kisha watayapatia ufumbuzi tofauti na utaratibu wa zamani wa kupokea taarifa zilizoandikwa kwenye makaratasi. 

Makwinja alibainisha miongoni mwa malalamiko yanayotolewa mara kwa mara na wanufaika hao ni pamoja na kukatwa fedha zilizotokana na wao kushindwa kukidhi vigezo vilivyowekwa na mfuko. 

“Hapa ni lazina niseme kwamba sababu kubwa ni elimu kwa wanufaika maana wakati mwingine wanakiuka taratibu tulizoziweka hasa katika suala la elimu, afya na lishe, ” alisema Makwinja na kuongeza, 

“TASAF haigawi fedha tu kama wengi wanavyodhani, tunahaulisha kwa kutoa ruzuku kiasi kidogo cha fedha ili kuleta matokeo katika kaya masikini kwa kiwango kidogo wanachopewa, ” 

Alisema fedha hizo wanataka zilete tija kwa wanafamilia kwa watoto kwenda shuleni na kuhudhuria masomo kwa kiwango cha walau asilimia 80, kupata huduma za afya pamoja na lishe bora. 

Hata hivyo, ofisa huyo aliwataka watendaji waliopatiwa mafunzo hayo waone wajibu wa kile walichojifunza wakakitekeleze kwa kutumia ujuzi utakaosaidia mradi huo kuwa na kumbukumbu sahihi zitakazohifadhiwa kwa njia ya eletroniki. 

Hadi sasa mfuko wa Tasaf umeweza kuhudumia Kaya masikini zipatazo milioni moja na laki moja nchini kupitia mpango huo (SDGs). 

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

spot_img

Related articles

EMERY APANGA KUIBOMOA BARCELONA

LONDON, Uingereza KOCHA wa Aston Villa, Unai Emery, anaitaka saini ya beki wa Barcelona, Alejandro Balde, na amewaambia mabosi...

BAYERN YAMKODOLEA MACHO KIUNGO WA TOTTENHAM

LONDON, Uingereza BAYERN Munich inampigia hesabu za karibu kiungo wa Tottenham na timu ya Taifa ya Senegal, Pape Matar...

RIPOTI: IDADI YA WAHAMIAJI ULAYA IMEVUNJA REKODI, UJERUMANI INAONGOZA

LONDON, UingerezaRIPOTI mpya imeonesha kuwa Ulaya nchi za Ulaya zlipokea wahamiaji milioni 64 mwaka 2025, likiwa ni ongezeko...

RAIS WA TAIWAN ASITISHA ZIARA YAKE AFRIKA, CHINA IKITAJWA KUWA CHANZO

TAIPEI, TaiwanRAIS wa Taiwan, Lai Ching-te, ameahirisha ziara yake nchini Eswatini, huku akiitaja China kuwa ndiyo chanzo cha...