RAIS SAMIA ATANGAZA SIKU YA SENSA NI MAPUMZIKO

Date:

Share post:

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa


RIPOTA WA WAZIRI MKUU

WAZIRI Muu, Kassim Majaliwa amesema Rais Samia Suluhu Hassan ameridhia tarehe 23 Agosti, ambayo ni siku ya sensa na makazi ya watu iwe ni siku ya mapumziko.


Akizungumza katika kikao cha saba cha Kamati Kuu ya Taifa ya Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022 kilichofanyika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam, alisema Rais Samia ameridhia hilo ili Watanzania wawepo majumbani kuwapokea makarani wa sensa.

“Ninapenda kuwajulisha wajumbe wa kikao hiki kwamba Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan ameridhia tarehe 23 Agosti iwe ni siku ya mapumziko ili Watanzania wawepo majumbani, waweze kuwapokea makarani wa sensa na kutoa maelezo husika,” amesema.

Alisema kutokana na uamuzi huo anaamini sensa ya watu na makazi itafanyika vizuri kama ilivyopangwa.

 

Mapema, Waziri Mkuu alipokea vishkwambi 600 kutoka kwa Balozi wa Korea Kusini, Kim Sun Pyo vyenye thamani ya shilingi milioni 202. Pia alipokea fulana 1,759 zenye ujumbe wa kuhamasisha sensa zenye thamani ya sh. milioni 20 kutoka kwa Mkuu wa Kitengo cha Taasisi za Serikali wa Benki ya NMB, William Makoresho ambaye alikabidhi kwa niaba ya mtendaji mkuu wa benki hiyo.

Wajumbe wa kikao hicho walijulishwa kwamba utafiti uliofanywa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) umebainisha kuwa uelewa wa wananchi kuhusu sensa umefikia asilimia 99 ikilinganishwa na asilimia 96 ya Juni, 2022.

 

 

 

About The Author

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

spot_img

Related articles

UCHUMI WA CHINA WAZIDI KUIMARIKA

BEIJING, China LICHA ya vita vya Marekani na Iran kuonekana kuitikisa dunia, China imeendelea kupiga hatua kubwa katika eneo...

SIKU 100 ZA RAIS MPYA WA VENEZUELA: MABADILIKO NA MASWALI MAPYA

CARACAS, Venezuela BAADA ya vikosi vya Marekani kumng’oa madarakani aliyekuwa Rais wa Venezuela, Nicolás Maduro kwenye oparesheni ya Januari...

MAELFU YA FAMILIA SUDAN BADO WAKIMBIA VITA, HALI YA MAISHA YAZIDI KUWA MBAYA

MAELFU ya familia nchini Sudan bado wanalazimika kuyakimbia makazi yao, miji na hata mipaka ya nchi kufuatia vita...

ISRAEL YAENDELEA NA OPERESHEN DHIDI YA HEZBOLLAH NCHINI LEBANON

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema Jeshi la nchi yake linaendelea na operesheni dhidi ya wanamgambo wanaoungwa...