TEMESA KUANZA KULIPA MADENI YA WAZABUNI

Date:

Share post:

 

Wazari Mkuu, Kassim Majaliwa

NA MWANDISHI WETU

WAKALA wa Ufundi na Umeme (TEMESA), itaanza kulipa sehemu ya madeni ya shilingi bilioni nne wanayodai wazabuni kutokana na fedha zilizolipwa na wizara na idara za serikali zilizotokana na agizo la Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.

Wazabuni mbalimbali wanaidai TEMESA fedha za kusambaza vipuli na vilainishi pamoja na kutengeneza magari ya wizara na idara za serikali, madeni yanayofikia shilingi bilioni nne ya tangu 2012.

Akizungumza na Tanzania PANORAMA Blog, Mtendaji Mkuu wa TEMESA, Dk. Stephen Massele alisema baada ya malalamiko ya muda mrefu kutoka kwa wazabuni,  sasa wataanza kulipa baada ya kukamilisha upitiaji wa madeni kwa kila mzabuni.

Dk. Massele alisema baadhi ya wazabuni ikiwemo kampuni ya Planet mawakili wao,  wamekwishapewa taarifa kwamba TEMESA inafanya mapitio ya madeni na itaanza kulipa  baada ya wiki moja.

Alisema fedha zitakazolipwa zimetokana na madeni wanayodai wizara na idara za serikali zilizopata huduma ya wazabuni hao na zitalipwa kama ilivyoagizwa na Waziri Mkuu mapema mwanzoni mwa mwaka huu.

Dk. Masele alisema madeni mengine ya wazabuni hao, yataendelea kulipwa kulingana na upatikanaji wa fedha kutoka kwa wadeni wao. TEMESA inazidai wizara na idara za serikali kiasi cha shilingi bilioni tano.

“Baadhi ya wazabuni tumewapa maelekezo kupitia mawakili wao,  wapo waliotuelewa kuwa tunakamilisha ‘Reconciliation’ ya fedha zilizolipwa kwa agizo la Waziri Mkuu nani ana fedha ya madeni yake na ndani ya wiki moja tutakamilisha malipo yake, ” alisema Dk. Massele na kuongeza.

“Ambayo hayajalipwa hiyo watapewa taarifa na mameneja husika mengine yatasubiri kadiri tunavyolipwa. “

Kauli hiyo ya Dk. Masele imetolewa baada ya kuwepo malalamiko ya muda mrefu ya wazabuni kupitia viongozi wao wa Umoja wa Gereji Tanzania (UGETA).

Akizungumza na Tanzania PANORAMA, Mwenyekiti wa Umoja wa Gereji Tanzania (UGETA), Lumona Mkala, alisema wanachama wake wanaidai TEMESA MT Depot zaidi ya shilingi Bilioni nne za kusambaza vipuli na vilainishi vya mafuta ya magari.

Alitaja wazabuni wanaodai ni Beka investment shilingi  250,563,150, Moroturbo shilingi 80,256,197, Planet Busines link shilingi 175,312,570 na Ndeken shilingi 194,801,393

Wengine ni Kigustar Enterprisess,  Leonardo Automotive Garage, Nedea Enterprisess, RaaR Investment, Kigoma Garage, Adam Motor na Point A.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

spot_img

Related articles

RAIS WA TAIWAN ASITISHA ZIARA YAKE AFRIKA, CHINA IKITAJWA KUWA CHANZO

TAIPEI, TaiwanRAIS wa Taiwan, Lai Ching-te, ameahirisha ziara yake nchini Eswatini, huku akiitaja China kuwa ndiyo chanzo cha...

USIYOYAJUA KUHUSU ZIARA YA PAPA LEO BARANI AFRIKA

KIONGOZI wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Leo XIV, yuko barani Afrika kwa ziara ya siku 10 katika mataifa...

MATESO WANAYOPITIA WATOTO KATIKA MACHAFUKO YA SUDAN

DARFUR, Sudan "HALI ya watoto nchini Sudan inazidi kuwa mbaya kila baada ya saa moja." Hiyo ni kauli ya...

IRAN: TUKO TAYARI KWA VITA MAZUNGUMZO YAKISHINDIKANA

TEHRAN, IranSPIKA wa Bunge la Iran, Mohammad Bagher Ghalibaf, amesema nchi yake itakuwa tayari kwa mbinu mpya za...