Monday, June 23, 2025
spot_img

NGUVU YA BUNGE YAJARIBIWA NA CC YA CHADEMA

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe akizungumza katika mkutano wa ndani wa Chadema

 NA MWANDISHI WETU

HATIMAYE imebainikiwa kuwa uamuzi wa Kamati Kuu (CC) ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kuwavua uanachama makada wake 19 wanawake, kinaowatuhumu kwa utovu wa nidhamu na kula kiapo cha kuwa wabunge wa viti maalumu bila kupitishwa na chama ni mwendelezo wa matukio yake ya ‘kisanii’

Hayo yameelezwa na wataalamu bingwa wa mambo ya kibunge, Wataalamu wa Katiba, Wanasheria nguli wa Sheria za Uchaguzi na maafisa wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) katika mahojiano maalumu na Tanzania PANORAMA Blog kuhusu hatua ya Kamati Kuu ya Chadema kuwavua ubunge makada wake hao na uhalali wa uamuzi wa Spika kuwaapisha nje ya ukumbi wa Bunge.

Mmoja wa watalaamu waliobeba katika mambo ya mabunge ya Jumuiya ya Madola ambaye ni mshauri na mkufunzi wa kanuni, utamaduni, utaratibu na mienendo wa mabunge barani Afrika ameeleza kuwa uamuzi wa Kamati Kuu ya Chadema ni mchezo wa kisiasa wenye lengo la kukirudisha chama hicho midomoni na masikioni mwa watanzania wakati huu kinapoelekea kutoweka.

Alisema kisheria, kikanuni na utamaduni wa mabunge wa Jumuiya ya Madola, wabunge 19 wanawake wa viti maalumu wa Chadema hawana kosa lolote katika mchakato mzima uliowezesha kuapishwa kwao hivyo hawapaswi kuhukumiwa kwa namna yoyote ile.

Alisewa mbali na wabunge hao, Spika wa Bunge, Job Ndugai pia hana kosa kwa sababu hajakiuka sheria na kanuni za Bunge kuwaapisha wabunge hao na wala hajatenda kinyume na tamaduni na taratibu za kibunge ambapo Bunge la Tanzania linafuata mfumo wa kiuendeshaji wa mabunge ya Jumuiya ya Madola.

Halima Mdee akiapa mbele ya Spika wa Bunge, Job Ndugai


Alisema kabla ya kuapishwa kwa wabunge hao kulikuwa na mawasiliano ambayo kisheria ni ya siri baina ya chama cha siasa husika na Tume ya Taifa ya Uchaguzi yaliyohusu uwasilishaji na upokeaji wa orodha ya watu wenye sifa za kuwa wabunge, orodha ambayo baada ya kupokelewa na NEC, ilifanyiwa kazi kisha ikawasilishwa kwa Spika.

“Kwa mujibu wa sheria, katibu mkuu wa chama ndiyo mwenye jukumu la kuwasilisha majina NEC na kwa maelezo ya NEC hilo lilifanyika. Na mawasiliano kati ya chama cha siasa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuhusu chama kuwasilisha orodha ya majina ya watu wenye sifa kuwa wabunge wa viti maalumu na tume kuyapokea na kuyafanyia kazi huwa siri.

“Yakishafanyiwa kazi na NEC ndiyo humjulisha Spika na yeye huendelea na taratibu za kibunge.

“Wakati hayo yakitendeka baina ya Katibu Mkuu wa Chadema na NEC, wabunge hawakupewa fursa ya kujua mawasiliano yaliyofanyika na hawakupaswa kujua. Baada ya hilo walijulishwa na chama chao kuwa wameteuliwa kuwa wabunge na walipaswa kuripoti bungeni.

Mkurugenzi wa NEC, Charles Mahela


“Spika yeye alipokea barua tu toka NEC kumjulisha juu ya uteuzi huo na ndiyo utaratibu ulivyo, Spika hutaarifiwa na NEC. Sasa mpaka hapo wabunge hao 19 na Spika hawawa kosa lolote.

“Labda kama NEC ingesema aliyeandika barua siyo katibu mkuu na kwa hiyo orodha ya Chadema isingepokelewa lakini NEC imesema wazi katika tamko lake kuwa orodha hiyo ilitoka Chadema.

“Kwa hiyo Chadema iweke wazi na ijibu kauli ya NEC kuwa wao ndiyo waliandika barua na kuwasilisha orodha ya wabunge wa viti maalumu bila kuwa na sharti la namna walivyopatikana kwa sababu siyo hitaji la NEC kujua, badala ya kumshambulia Spika na kudhalilisha wabunge waliokwishaapishwa” alisema mtaalamu huyo wa mambo ya kibunge ya Jumuiya ya Madola.

Mbali na huyo, mwanasheria nguli wa sheria za uchaguzi na masuala ya Katiba ambaye naye hakupenda kutajwa jina lake, yeye alisema wabunge 19 wa viti maalumu wa Chadema hawawezi kutengua kiapo chao na uamuzi wa Kamati Kuu ya Chadema hauwazuii kuendelea kutekeleza majukumu yao ya kibunge.

Spika wa Bunge, Job Ndugai


“Mambo ya hicho chama sipendi kuyaongelea kisheria kwa sababu kila siku wanaibuka na jambo. Lakini nitakueleza kisheria ilivyo ila sitaki kuandikwa jina mimi kwa sababu sihitaji kuingia kwenye malumbano ya kisanii na hao watu. Naeleza kuwajuza watanzania.

“Kwa namna yoyote ile wabunge 19 wa viti maalumu wa Chadema wataendelea na wajibu wao, sioni sababu ya kutengua kiapo chao.

“Kuapa nje ya Bunge ni sharti jipya la kikanuni kwa wabunge waliochelewa kuapa kabla ya ufunguzi wa Bunge na Spika mwenyewe amekwishalitolea ufafanuzi na lipo ndani ya kanuni za Bunge labda kama hao Chadema hawasomi kanuni.

“Kwa msingi huo sharti hilo linapata nguvu ya ibara ya 89 ya Katiba kwa kutunga Kanuni za Bunge na ndiyo uwepo wa kanuni hiyo mpya.

“Lakini Pia anayetuhumu ndiyo mwenye jukumu la kuthibitisha pasipo shaka kuwa barua ile siyo yao na siyo ya NEC. Chadema watoke wakanushe kama barua iliyopo NEC siyo ya kwao.

“Upo ushahidi wa kutosha kuwa Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika aliwasilisha barua ya orodha ya wabunge wa viti maalumu kwa rejista na mawasiliano ya simu na ofisi ya NEC baada ya kuomba ajulishwe rasmi kwa barua sharti la kuwasilisha orodha ya majina ya wabunge wa viti maalumu,” alisema ngwiji huyo wa Sheria za Uchaguzi na Mambo ya Katiba.

Alitoa mfano kuwa kinachofanya na Chadema ni sawa sawa na mbunge aliyetambulishwa na chama chake kuwa mgombea, baada zoezi la uchaguzi anapopewa hati ya kutangazwa kuwa mbunge na baadaye kwenda kula kiapo anafukuzwa na chama chake.

Nyingine Zinazohusiana na Hii

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Tufuatilie

0FansLike
3,913FollowersFollow
0SubscribersSubscribe
- Advertisement -spot_img

Habari Nyingine Mpya