SIMBA, FISI WALISHWA SUMU

Date:

Share post:

MACHI 3, 2013
kundi la Simba
DODOMA
Simba sita na Fisi zaidi ya 100 wamekufa baada ya kulishwa simu iliyowekwa kwenye nyama pembezoni mwa Hifadhi ya Ruaha.
Pamoja na wanyama hao, ndege zaidi 100 nao wamekufa baada ya kula mizoga ya Simba na Fisi iliyowekewa sumu na wafugaji, wiki tatu zilizopita.
Mauaji hayo ya wanyama wamebainishwa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamis Kigwangalaah alipokuwa akizungumza katika maadhimisho ya siku ya wanyamapori duniani mjini hapa.
Kundi la Fisi

Akizungumza katika maadhimisho hayo, Waziri Kigwangallah alieleza kusitikishwa na mauaji hayo ya wanyama na ndege aliyoyaita kuwa ya kulipiza kisasi.
Alionya kuwa Serikali itachukua hatua kali kwa watu wanaoua wanyama jamii ya paka wakubwa kwa sababu wapo katika hatari ya kutoweka.
Alisema, wakati  wanyama wa jamii ya paka wakubwa wakiwa katika hatari ya kutoweka, Faru na Tembo wamekuwa katika hatari hiyo kwa muda mrefu.
Kwa mujibu wa takwimu za Taasisi ya Wanyapori (Tawiri) Tanzania kuna Simba 16,800, Chui 25,000 na Duma 1180.
Biashara ya utalii hapa nchini inachangia asilimia 18 ya pato la taifa na asilimia 25 ya fedha za kigeni huku akitoa ajira  kwa watu 500,000 za moja kwa moja na ajira zisizokuwa za moja kwa moja zaidi ya milioni mbili.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

spot_img

Related articles

SOMA HIYO! ISRAEL NDIYO WAASISI WA MIKWAJU YA PENALTI

LONDON, Uingereza NI jioni ya Agosti 5, 1970 kwenye Uwanja wa Boothferry Park mjini Hull, Manchester United ikiwa ugenini...

AMEJIPATA! LAMPARD ALIVYOREJEA EPL AKIWEKA REKODI

LONDON, Uingereza IKIWA ni miezi 18 tu imepita tangu alipoajiriwa, Frank Lampard ameiwezesha Coventry City kupanda daraja na kurejea...

USICHUKULIE POA! PATORANKING ALIUZA SUMU YA PANYA MITAANI KABLA YA ‘KUTOBOA’

LAGOS, Nigeria WAHENGA walisema maisha ni safari yenye milima na mabonde. Kwamba katika kuishi kwako, si nyakati zote zitakuwa...

KIFO CHA BOSI KINAVYOITESA LEICESTER CITY

LONDON, UingerezaMIAKA 10 iliyopita, Leicester City waliishangaza dunia walipotwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya England (EPL) mbele ya...