‘WANASIASA MWACHENI AKWILINA APUMZIKE KWA AMANI’

Date:

Share post:

MACHI 3, 2018

DODOMA
Wanasiasa wameonywa waache kuutumia kisiasa msiba wa mwanafunzi Akwilina Akwilini ili apumzike kwa amani.
Akwilina aliuawa mwezi uliopita baada ya kupigwa risasi wakati polisi wakitawanya  maandamano ya wanachama na mashabiki wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)
Mbali na wanasiasa, wengine walioonywa kuacha kuutumia msiba huo kwa malengo yao ni makundi yote yanayotumia mwamvuli wa wanasiasa.
Onyo hili limetolewa jana na Mwenyekiti Jumuiya ya Taasisi za Vyuo vya Elimu ya Juu Tanzania (TAHLISO) George Mnali katika mkutano wa tamati tendaji ya umoja huo.
Kamati hiyo iliketi jana kujadili changamoto zinazowakabili wanafunzi wa vyuo vikuu.
Alisema TAHLISO inaelekeza lawama kwa makundi matatu kwa tukio hilo aliyoyataja kuwa ni  wanasiasa, wananchi na waliozuia maandamano hayo ambayo yaligharimu uhai wa Akwilina.
Alisema wanasiasa wanapaswa kuchunga kauli
zao, waangalie wanazungumza nini na wapi kwa sababu taifa linataka amani.
Mnali alisema onyo hilo halilenga kundi lolote la wanasiasa bali linawahusu wote.Akizungumza lawama kwa wananchi alisema wanapaswa kujitafakari wenyewe kabla ya kutekeleza kitendo chochote wanachoambiwa kukifanya.
Na kuhusu waliozuia maandamano, alisema walipaswa kuwa makini kwa sababu katika maandamano yale kilichotakiwa ni kuzuia tu.
“TAHLISO  ndio chombo kikuu cha kuwasemea wanafunzi wote nchi nzima, hakuna mwingine.
“Tambua kuna kifo cha mwanafunzi mwenzetu Akwilina aliyekuwa anasoma Chuo cha Usafirishaji lakini kuna vikundi vimejitokeza kutoa matamko mbalimbali.
“Vikundi vingine vimeenda mbali zaidi kwa kuwataka baadhi ya watendaji kujiuzulu wakati uchunguzi bado unaendelea na matokeo
hayajatoka, inaashiria vinatumika kisiasa,” alisema Mnali.

Previous article
Next article

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

spot_img

Related articles

SOMA HIYO! ISRAEL NDIYO WAASISI WA MIKWAJU YA PENALTI

LONDON, Uingereza NI jioni ya Agosti 5, 1970 kwenye Uwanja wa Boothferry Park mjini Hull, Manchester United ikiwa ugenini...

AMEJIPATA! LAMPARD ALIVYOREJEA EPL AKIWEKA REKODI

LONDON, Uingereza IKIWA ni miezi 18 tu imepita tangu alipoajiriwa, Frank Lampard ameiwezesha Coventry City kupanda daraja na kurejea...

USICHUKULIE POA! PATORANKING ALIUZA SUMU YA PANYA MITAANI KABLA YA ‘KUTOBOA’

LAGOS, Nigeria WAHENGA walisema maisha ni safari yenye milima na mabonde. Kwamba katika kuishi kwako, si nyakati zote zitakuwa...

KIFO CHA BOSI KINAVYOITESA LEICESTER CITY

LONDON, UingerezaMIAKA 10 iliyopita, Leicester City waliishangaza dunia walipotwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya England (EPL) mbele ya...