Tuesday, 13 October 2026

111 AKIWAMO DIWANI WAPUKUTIKA CHADEMA

Gervas Mwakyusa muda mfupi baada ya kusajili wa CCM akitokea Chadema   MACHI 4, 2018 Wanachama 110 wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), wamekihama chama hicho leo na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM). Sambamba nao, Garvas Mwakyusa, Diwani wa  Kata ya Legezamwendo katika Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo, Mkoa wa Rukwa kwa tiketi ya […]
Gervas Mwakyusa muda mfupi baada ya kusajili wa CCM akitokea Chadema  

MACHI 4, 2018

Wanachama 110 wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), wamekihama chama hicho leo na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Sambamba nao, Garvas Mwakyusa, Diwani wa  Kata ya Legezamwendo katika Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo, Mkoa wa Rukwa kwa tiketi ya Chadema naye amejivua wadhfa wake pamoja na uanachama na kujiunga na CCM.
Taarifa kutoka mkoani Rukwa zimeeleza kuwa tukio hilo limetokea katika mkutano wa ndani wa CCM wa ujenzi wa chama katika Wilaya ya Kalambo ulioongozwa na Katibu Mwenezi wa CCM, Taifa Humphrey Polepole.
Katibu Mwenezi wa CCM, Humphrey Polepole akizungumza katika mkutano wa ndani kwenye Kata ya Lugezamwendo wilayani Kalambo, leo.

Umati wa wananchi waliohudhuria mkutano huo

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *