MACHI 5, 2018
Dk. Mpoki |
DAR ES SALAAM
Maneno nusu kaputi yanalotumiwa na watalaamu wa dawa za usingizi yanamaanisha kumuua mtu nusu na nusu nyingine anabaki akiwa hai.
Tafasili ya maneno hiyo imetoleana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Mpoki Ulisubisya alipokuwa akifungua mafunzo ya awamu ya tatu kwa wataalamu wa dawa za usingizi jijini Dar es Salaam leo.
Dk Mpoki alisema neno hilo ni baya kwa sababu linawaogopessha wagonjwa wanaotakiwa kufanya upasuaji ambao ni lazima wapatiwe dawa hiyo ya usingizi.
Aliwashauri watalaamu hao kuwa, badala ya kutumia maneno nusu kaputi watumie maneno tiba ya dawa za usingizi.
Alisema msingi wa kuwataka wasitumie maneno nusu kaputi na badala yake watumie maneno tiba ya dawa ya usingizi ni kwa sababu mtu anapopewa dawa ya usingizi huwa analala na baadaye huamka lakini hauawi nusu na nusu nyingine kubaki akiwa hai.
 “Dawa ya kulaza wagonjwa au dawa ya usingizi inatolewa ili mgonjwa anapofanyiwa upasuaji asisikie maumivu anapokatwa mwilini, hivyo siyo sahihi kusema mgonjwa kauawa nusu na nusu kaachwa akiwa hai” alisema Dk. Mpoki..