Karia |
DAR ES SALAAM
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF), Wallace Karia ameitisha mkutano na wahariri wa habari za michezo, leo.Mkutano huo unatarajiwa kufanyika katika Hotel ya Sea Scape, iliyopo Dar es Salaam saa 4.00 asubuhi.
Inatarajiwa kuwa, Rais Karia atautumia mkutano huo kutoa ufafanuzi wa tuhuma ambazo Makamu wa Rais wa TFF, Michael Wambura amezielekeza kwa taasisi anayoiongoza.
Aidha, haina shaka kuwa Rais Karia atautumia mkutano huo kuzungumzia kwa kina uamuzi wa kumfungia milele, Wambura kutojihusisha na shughuli za michezo.Â