DAR ES SALAAM
Mjadala mpya umeibuka nchini baada ya Makamu wa Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuadhibiwa kutojihusisha na soka milele.
Wambura anatuhumiwa kughushi nyaraka na kuchukua fedha kinyume cha taratibu.
Lakini Wambura amepaza sauti akisema kwanza waliomuadhibu hawana mamlaka hayo lakini pia hatua hiyo imefikiwa kwa sababu ya kukemea maovu ndani ya TFF?
Wambura amekaririwa kuwa alihoji matumizi mabaya ya fedha za TFF.
Wambura |
Kwamba yeye (Wambura) akiwa Mwenyekiti wa Kamati ya Fedha ya TFF alihoji matumizi mabaya ya shirikisho hilo linalodaiwa kutumia kiasi cha sh. bilioni 3 kwa muda wa miezi saba kwa ajili ya maendeleo ya soka Tanzania
 Kwamba Wambura hakuridhishwa na alihoji mwenendo wa utoaji ajira ndani ya TFF. Inadaiwa kuna upndeleo katika utoaji ajira na zabuni za utoaji ajira hazitangazwi.
Kwamba wafanyakazi wengi wameajiriwa kiushikaji bila kufuata taratibu na kanuni za TFF. Inatajwa moja ya ajira hizo ni ya Kaimu Katibu wa TFF (Wilfred Kidao) na Afisa Habari wa TFF (Criford Ndimbo)
Wambura anadai kuwa kumteua Wilfred Kidao kuwa Kaimu Katibu wa TFF ni kinyume cha taratibu na kwamba waliostahili ni mmoja kati ya maofisa wa TFF.
Kwamba taratibu zinataka afisa aliye ndani ya TFF kukaimu na sio kuteua mtu yoyote ambaye hakuwa afisa wa TFF.
Kwamba kuna watu wamepiga fedha za TFF kwani kuna mipira imeandikiwa fedha kubwa bila uhalisia kwani mipira hiyo haiwezi kutumika hata wiki bila kuharibika.
Kwamba TFF kwa sasa kama Rais, Nyamlani na Mgoyi hawakutaki unatoka. Kuna nafasi za kazi TFF watu wameajiriwa wapya wakati wa zamani wana mikataba na TFF na TFF inaingia hasara ya kulipa mishahara mara mbili.
Uchunguzi wa tuhuma hizi unakujia hivi karibuni.