MSIDANGANYIKE KUHUSU BEI YA KAHAWA – MAJALIWA

Date:

Share post:

 

NA MWANDISHI WETU

MJUMBE wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Kassim Majaliwa amesema serikali imedhamiria kuhakikisha kilimo kinamnufaisha mkulima wa Tanzania. 

“Watu wasije kuwadanganywa kwamba serikali haiwajali, siyo kweli. Kuna sababu zilizochangia kuyumba kwa bei ya kahawa kwenye soko la dunia.”

Ametoa kauli hiyo leo mchana alipokuwa  akizungumza na wakazi wa Rubale katika mkutano uliofanyika kwenye viwanja vya Shule ya Msingi Rubale, wilayani Bukoba, mkoani Kagera.

“Serikali ya awamu ya tano ilipoingia madarakani, iliazimia kufufua mazao matano ya kimkakati ambayo ni kahawa, pamba, korosho, chai na tumbaku. Mazao haya bei ilishuka na si katika zao la kahawa tu.

“Kuyumba kwa bei haikuwa katika zao la kahawa tu bali katika mazao mengine kama pamba na korosho. Kahawa bei yake iliathirika kwa sababu ya ugonjwa wa Corona. Korosho bei ilishuka kutoka sh.3,300 hadi sh. 1,900. Pamba pia ilishuka bei,” amesema. 

Amesema Kenya ndiko mnada wa kahawa huwa unafanyika lakini hadi sasa bado wanasumbuliwa na ugonjwa wa Corona kwa hiyo haikuwa rahisi kufanya biashara katika kipindi chote hicho.

Majaliwa ambaye ameanza ziara katika Mkoa wa Kagera kumuombea kura mgombea irais kwa tiketi ya CCM, Dk. John Pombe Magufuli ametumia fursa hiyo kuwaombea kura mgombea ubunge kwa tiketi ya CCM, Jason Rweikiza, mgombea udiwani wa kata ya Rubale, Rwegasira Renatus Rwechungura na madiwani wengine wa jimbo hilo.

Kuhusu maji, amesema sh. bilioni 4.09 zilitolewa ili kuboresha miradi ya maji katika vijiji kadhaa ambayo yote imekamilika. Almevitaja vijiji hivyo kuwa ni  Ibwera, Kasharu, Kitahya, Katale, Itongo, Bituntu, Kibona, Katoro, Mikoni, Kibirizi Ngarama, Ruhoko na Ruhunga

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

spot_img

Related articles

JELA MIAKA 30 KWA KUPATIKANA NA BANGI

MAHAKAMA ya Wilaya ya Kyela mkoani Mbeya imemhukumu Brown Frank Mwaitubi (31), mkazi wa Kajunjumele, kifungo cha miaka...

DUTERTE KUPANDISHWA KIZIMBANI ICC

MANILA, Ufilipino JOPO la majaji watatu wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) limethibitisha kuwa Rais wa zamani wa...

WRIGHT: RICE APEWE BALLON D’OR

LONDON, Uingereza MKONGWE wa Arsenal, Ian Wright, amemtaja Declan Rice kuwa anastahili kutwaa tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwaka...

ISRAEL, LEBANON ZAONGEZA WIKI TATU ZA KUSITISHA VITA

WASHINGTON DC, Marekani RAIS wa Marekani, Donald Trump, amesema Israel na Lebanon zimekubaliana kuongeza wiki tatu za kusitisha mapigano. Wakati...