MWANAMUZIKI MISRI AFUNGWA KWA KUKASHIFU MTO NILE

Date:

Share post:

RIPOTA MAMALUMU
MWANAMUZIKI maarufu wa Misri, Sherine Abdel Wahab amehukumiwa kifungo cha miezi sita gerezani kwa kukashifu usafi wa Mto Nile.

Sherine ambaye pia ni jaji katika kipindi cha mashindano ya waimbaji yanayojulikana kwa jina la The Voice, alitiwa hatiani na mahakama wiki hii baada ya kushitakiwa kwa kosa la kuukashifu Mto Nile.

Ilidaiwa mahakamani kuwa mwanamuziki huyo aliwaambia wapenzi na mashabiki wake wakati wa onyesho lake nchini humo kwamba kunywa maji ya Mto Nile kunaweza kumpatia vijidudu.

Sherine alifunguliwa mashitaka mwezi Novemba mwaka jana baada ya video yake kusambazwa mtandaoni ikimuonyesha akiombwa kuimba wimbo uitwao Mashrebtesh Men Nilha (umewahi kunywa maji ya Mto Nile?).

Katika video hiyo, Sherine alionekana akiwajibu wapenzi na mashabiki wake kuwa ‘Nikinywa maji ya Mto Nile nitapata kichocho.’

Nchini Misri, ugonjwa wa kichocho unawapata zaidi wananchi wa vijijini. Aidha, chama cha wanamuziki nchini Misri kimetangaza kuupiga marufuku wimbo huo kuibwa nchini humo.

Wakati huo huo, mwanamuziki mwingine, Laila Amer naye mapema wiki hii alihukumiwa kifungo cha miaka miwili gerezani baada ya kupatikana na hatia ya uchochezi, ufitini na uovu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

spot_img

Related articles

GUARDIOLA AMPONZA KOCHA WA BURNLEY

LONDON, Uingereza KOCHA wa Burnley, Scott Parker, amekalia kuti kavu baada ya timu hiyo kufungwa bao 1-0 na Manchester...

BERNARDO AWEKA REKODI MPYA MAN CITY

MANCHESTER, Uingereza KATIKA ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Burnley, kiungo wa Manchester City, Bernardo Silva, ameweka rekodi ya...

MABOSI WAMTAKA BRUNO KUBAKI UNITED

MANCHESTER, Uingereza UONGOZI wa klabu ya Manchester United uko tayari kufanya lolote ili kumbakiza kiungo wake raia wa Ureno,...

CESC FABREGAS KOCHA MPYA CHELSEA?

LONDON, Uingereza KLABU ya Chelsea inaangalia uwezekano wa kumkabidhi benchi la ufundi kiungo wao wa zamani raia wa Hispania,...