MAISHA YA WAANDISHI WA HABARI KATIKATI YA VITA NCHINI IRAN

Date:

Share post:

TEHRAN, Iran
KWA miaka mingi, Iran imekuwa na taswira mbaya linapokuja suala la uhuru wa vyombo vya habari, ikishika nafasi ya 177 katika nchi 180 duniani, kwa mujibu wa Ripoti ya Mwaka 2026 ya Waandishi Wasio na Mipaka (RSF).

Hata hivyo, vita vyake dhidi ya Marekani na Israel vimetajwa kuongeza mazingira magumu kwa tasnia ya habari.

Taarifa zinaeleza kuwa hali ya vyombo vya habari kupangiwa namna na aina ya habari za kuripoti imeongezeka mara dufu tangu kuanza kwa vita hivyo Februari 28, 2026.

Mbaya zaidi, ni baadhi tu ya vyombo vya habari vyenye ‘uhusiano mzuri’ na mamlaka ndivyo vinavyopewa ruhusa ya kuvuka mipaka na kuifikia hadhira ya nje ya nchi.

Machi, 2026, RSF iliripoti kuwa waandishi wa habari wa Iran, ambao kwa namna moja au nyingine wameonekana kukosoa serikali, wamekuwa wakipokea simu za vitisho.

Kwa mujibu wa ripoti, mamlaka zimekuwa zikidhibiti upatikanaji wa mtandao (intaneti) tangu Januari 8, 2026, kabla ya vita vyake na Marekani kuanza.

Walau mamlaka zililegeza kamba wakati fulani, kabla ya kuzima tena intaneti baada ya vita kuanza Februari 28.

Huku wananchi wa kawaida wakikosa kabisa, intaneti imekuwa ikipatikana kwa baadhi tu ya vyombo vya habari, ambao vimeonekana kuiunga mkono Serikali.

Kwa waandishi wachache wanaotumia intaneti, wanalazimika kuwa na kadi za simu (laini) maalumu zinazotolewa kwa kibali cha mamlaka.

Behrouz Turani, ambaye ni mwandishi mkongwe aliyefanya kazi na vyombo vya habari vya ndani na nje ya Iran, anasema waandishi wamelazimika kuripoti kile kinachotakiwa na mamlaka.

“Hii imesababisha kuwapo kwa tofauti kubwa kati ya kinachoripotiwa na hali halisi ya mateso wanayopitia wananchi wa Iran wakati huu wa vita,” amesema.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

spot_img

Related articles

KISWAHILI KUIMARISHWA NCHINI KUELEKEA MICHUANO YA AFCON 2027

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda, amesema Serikali imeweka mkazo katika kuimarisha matumizi ya Kiswahili...

‘KARIAKOO DERBY’ YAVUNJA REKODI YA MABAO

BAADA ya sare ya mabao 2-2 jana Mei 3, 2026, mechi inayozikutanisha Simba na Yanga, maarufu kwa jina...

MASTAA WA KIGENI WAENDELEA KUTAMBA ‘KARIAKOO DERBY’

DAKIKA 90 za 'Kariakoo Derby' zilitamatika jana Mei 3, 2026 katika Uwanja wa Jenerali Isamhuyo jijini Dar es...

PANYA, NGUCHIRO WANAVYOTESA RAIA WA PALESTINA UKANDA WA GAZA

JERUSALEM, Palestina NI katika kambi za raia wa Palestina wanaoishi kwenye mahema baada ya makazi yao kusambaratishwa na mashambulizi...