MASTAA WA KIGENI WAENDELEA KUTAMBA ‘KARIAKOO DERBY’

Date:

Share post:

DAKIKA 90 za ‘Kariakoo Derby’ zilitamatika jana Mei 3, 2026 katika Uwanja wa Jenerali Isamhuyo jijini Dar es Salaam kwa vigogo wa soka, Simba na Yanga, kutoka sare ya mabao 2-2.

Katika mtanange huo wa 20 kwa kila timu msimu huu wa Ligi Kuu Bara, Simba ikiwa mwenyeji ilitangulia kwa mabao mawili, kabla ya Yanga ‘kujiuliza’ na kusawazisha yote na kuondoka na pointi moja.

Wekundu wa Msimbazi walipata mabao yao ya mapema kupitia kwa Libasse Gueye na Clatous Chama, wakati Yanga ilijinasua kupitia kwa Prince Dube na Bakari Nondo Mwamnyeto.

Kuziweka sawa takwimu, Gueye (Senegal), Chama (Zambia) na Dube (Zimbabwe) wameendeleza rekodi nzuri ya wachezaji wa kigeni kutamba katika mechi hizi za ‘derby’ ya Kariakoo.

Iko hivi; katika mechi saba zilizopita za Kariakoo Derby kati ya Simba na Yanga, yamefungwa jumla ya mabao 10, huku wachezaji wa kigeni wakiongoza kwa kuzifumania nyavu.

Michezo hiyo sita ya Ligi Kuu na mmoja wa Kombe la Muungano, imeshuhudia Yanga ikifunga mabao saba, wakati wenzao wa Msimbazi, Simba, wakiwa na matatu.

Kwa upande wa Yanga, mabao manne yalifungwa na wachezaji wa kigeni, Pacome Zouzoua (mawili), Maxi Nzengeli na Dube. Nyota hao wanatokea mataifa ya Ivory Coast, DRC na Zimbabwe.

Wachezaji wazawa walioifungia Yanga katika ‘derby’ saba za hivi karibuni ni Mzize, Kelvin Kijili (beki wa Simba aliyejifunga) na Mwamnyeto.

Simba, kwa upande wao, katika mabao matatu waliyoifunga Yanga, mawili yalipachikwa na wachezaji wa kigeni na moja la mchezaji mzawa.

Nyota hao wa kigeni ni Gueye na Chama, wakati mchezaji mzawa akiwa ni Seleman Mwalim aliyefunga bao pekee katika derby ya fainali ya Kombe la Muungano iliyochezwa hivi karibuni Visiwani Zanzibar.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

spot_img

Related articles

KISWAHILI KUIMARISHWA NCHINI KUELEKEA MICHUANO YA AFCON 2027

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda, amesema Serikali imeweka mkazo katika kuimarisha matumizi ya Kiswahili...

‘KARIAKOO DERBY’ YAVUNJA REKODI YA MABAO

BAADA ya sare ya mabao 2-2 jana Mei 3, 2026, mechi inayozikutanisha Simba na Yanga, maarufu kwa jina...

PANYA, NGUCHIRO WANAVYOTESA RAIA WA PALESTINA UKANDA WA GAZA

JERUSALEM, Palestina NI katika kambi za raia wa Palestina wanaoishi kwenye mahema baada ya makazi yao kusambaratishwa na mashambulizi...

MAPACHA WALIOZALIWA NA MAMA MMOJA LAKINI BABA TOFAUTI

LONDON, Uingereza MICHELLE na Lavinia Osbourne walipishana dakika chache tu kuzaliwa kwao. Ni mapacha waliotokana na mama mmoja lakini...