MAJERAHA YANAVYOMZUIA HAVERTZ KUWIKA ARSENAL

Date:

Share post:

LONDON, Uingereza

BALAA la majeraha lilianzia Februari, 2025, wakati Arsenal ilipokuwa Dubai. Kai Havertz alipata majeraha ya nyama za paja, akafanyiwa upasuaji uliomweka nje ya uwanja kwa miezi mitatu.

Katika mechi ya kwanza msimu huu, ambapo Arsenal waliifunga Manchester United, mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Ujerumani alipata majeraha mengine. Akawa nje ya dimba kwa miezi minne.

Tangu aliporejea, Havertz amepata majeraha mengine mawili kwa nyakati tofauti, likiwamo hili la hivi karibuni litakalomzuia kuivaa Atletico Madrid katika nusu fainali ya pili ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Havertz amecheza mechi 20 pekee msimu huu kutokana na mazingira hayo ya majeraha, moja pekee akiweza kumaliza dakika 90 ndani ya uwanja.

Mchezo aliomaliza dakika zote ni ule wa Arsenal kufungwa mabao 2-1 na Manchester United. “Sijawahi kuwa kwenye nyakati mbaya kiasi hiki,” alisema nyota huyo mwenye umri wa miaka 26.

Licha ya kukosekana kwake mara nyingi akiuguza majeraha, bado takwimu zinaonesha Havertz alivyo mchezaji muhimu katika kikosi cha Washika Bunduki wa London.

Katika mechi 20 tu alizoshuka dimbani, amehusika kwenye mabao tisa, akifunga matano na kutoa asisti nne. Ndiye aliyefunga bao lililoipeleka Arsenal hatua ya nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa.

Nyota huyo alitua Arsenal mwaka 2023 akitokea Chelsea, usajili wake ukigharimu Pauni milioni 65. Mkataba wake na klabu hiyo ya Kaskazini mwa London utakwisha mwaka 2028.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

spot_img

Related articles

KISWAHILI KUIMARISHWA NCHINI KUELEKEA MICHUANO YA AFCON 2027

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda, amesema Serikali imeweka mkazo katika kuimarisha matumizi ya Kiswahili...

‘KARIAKOO DERBY’ YAVUNJA REKODI YA MABAO

BAADA ya sare ya mabao 2-2 jana Mei 3, 2026, mechi inayozikutanisha Simba na Yanga, maarufu kwa jina...

MASTAA WA KIGENI WAENDELEA KUTAMBA ‘KARIAKOO DERBY’

DAKIKA 90 za 'Kariakoo Derby' zilitamatika jana Mei 3, 2026 katika Uwanja wa Jenerali Isamhuyo jijini Dar es...

PANYA, NGUCHIRO WANAVYOTESA RAIA WA PALESTINA UKANDA WA GAZA

JERUSALEM, Palestina NI katika kambi za raia wa Palestina wanaoishi kwenye mahema baada ya makazi yao kusambaratishwa na mashambulizi...