KISWAHILI KUIMARISHWA NCHINI KUELEKEA MICHUANO YA AFCON 2027

Date:

Share post:

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda, amesema Serikali imeweka mkazo katika kuimarisha matumizi ya Kiswahili katika michuano ya Mataifa ya Afrika (AFCON 2027) kwa kuandaa Istilahi maalumu 420 zitakazotumika katika shughuli mbalimbali za mashindano hayo.

Akiwasilisha bajeti ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa mwaka wa fedha 2026/2027 bungeni jijini Dodoma leo Mei 4, 2026, Waziri Makonda amesema hatua hiyo inalenga kuhakikisha Kiswahili kinatumika kwa ufasaha katika mawasiliano ya kimataifa kupitia michezo.

Aidha Ameeleza kuwa Istilahi hizo zimeandaliwa kwa ushirikiano na wataalamu wa lugha na taasisi husika ili kuendana na mahitaji ya kimataifa ya utangazaji, uandishi wa habari na mawasiliano ya michezo.

Sanjari na hayo Makonda amesema mpango huo pia ni sehemu ya kuendeleza hadhi ya Kiswahili kama lugha ya Afrika na dunia, hasa Tanzania ikiwa miongoni mwa wenyeji wa AFCON 2027.

Mbali na hayo Ameongeza kuwa Serikali itaendelea kuimarisha matumizi ya Kiswahili katika sekta zote ili kukifanya kiwe na ushindani zaidi katika anga la kimataifa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

spot_img

Related articles

‘KARIAKOO DERBY’ YAVUNJA REKODI YA MABAO

BAADA ya sare ya mabao 2-2 jana Mei 3, 2026, mechi inayozikutanisha Simba na Yanga, maarufu kwa jina...

MASTAA WA KIGENI WAENDELEA KUTAMBA ‘KARIAKOO DERBY’

DAKIKA 90 za 'Kariakoo Derby' zilitamatika jana Mei 3, 2026 katika Uwanja wa Jenerali Isamhuyo jijini Dar es...

PANYA, NGUCHIRO WANAVYOTESA RAIA WA PALESTINA UKANDA WA GAZA

JERUSALEM, Palestina NI katika kambi za raia wa Palestina wanaoishi kwenye mahema baada ya makazi yao kusambaratishwa na mashambulizi...

MAPACHA WALIOZALIWA NA MAMA MMOJA LAKINI BABA TOFAUTI

LONDON, Uingereza MICHELLE na Lavinia Osbourne walipishana dakika chache tu kuzaliwa kwao. Ni mapacha waliotokana na mama mmoja lakini...