BRUNO AWEKA REKODI UNITED IKIRUDI UEFA

Date:

Share post:

MANCHESTER, Uingereza

BAADA ya ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Liverpool jana Mei 3, 2026, Manchester United imefuzu kushiriki michuano ya Shirikisho la Soka la Ulaya (UEFA) ya Ligi ya Mabingwa msimu ujao.

Katika mchezo huo, nahodha Bruno Fernandes alihusika katika bao la ushindi la Kobie Mainoo, hivyo kuandika historia klabuni hapo.

Bruno anakuwa mchezaji pekee wa Man United aliyetengeneza nafasi nyingi (120) msimu huu, akivunja rekodi iliyodumu klabuni hapo tangu msimu wa 2003-04.

Mtanange huo uliishuhudia Man United ikipata mabao yake kupitia kwa Benjamin Sesko, Matheus Cunha na Mainoo.

Kwa sasa, Bruno amebakiza asisti moja kuifikia rekodi ya Thierry Henry na Kevin De Bruyne, ambao ndiyo wachezaji pekee kufikisha 20 ndani ya msimu mmoja wa Ligi.

Baada ya kujihakikishia nafasi ya kucheza Ligi ya Mabingwa msimu ujao, Man United itarejea dimbani Mei 9, 2026 kuikabili Sunderland, kabla ya kucheza na Nottingham Forest.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

spot_img

Related articles

KISWAHILI KUIMARISHWA NCHINI KUELEKEA MICHUANO YA AFCON 2027

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda, amesema Serikali imeweka mkazo katika kuimarisha matumizi ya Kiswahili...

‘KARIAKOO DERBY’ YAVUNJA REKODI YA MABAO

BAADA ya sare ya mabao 2-2 jana Mei 3, 2026, mechi inayozikutanisha Simba na Yanga, maarufu kwa jina...

MASTAA WA KIGENI WAENDELEA KUTAMBA ‘KARIAKOO DERBY’

DAKIKA 90 za 'Kariakoo Derby' zilitamatika jana Mei 3, 2026 katika Uwanja wa Jenerali Isamhuyo jijini Dar es...

PANYA, NGUCHIRO WANAVYOTESA RAIA WA PALESTINA UKANDA WA GAZA

JERUSALEM, Palestina NI katika kambi za raia wa Palestina wanaoishi kwenye mahema baada ya makazi yao kusambaratishwa na mashambulizi...