FEDHA ZA KUMWAGA KOMBE LA DUNIA 2026

Date:

Share post:

NYON, Uswis

MSIMU wa 23 wa fainali za Kombe la Dunia uko njiani, ukitarajiwa kufanyika kwa mwezi mmoja kuanzia Juni, 2026.

Ni fainali zitakazofanyika katika mataifa matatu (Marekani, Canada na Mexico) na kwa mara ya kwanza zitashirikisha timu 48 zinazowania ubingwa.

Kila timu inayoshiriki itaweka mfukoni Pauni milioni 1.1 za maandalizi, kisha kuongezwa Pauni milioni 7.7 za ushiriki.

Bingwa wa mashindano atakayepatikana Julai 19, 2026 katika Uwanja wa MetLife nchini Marekani atalamba Pauni milioni 36.9. Ni tofauti na Pauni milioni 31 walizopewa Argentina msimu uliopita (2022).

Wakati huo huo, timu iliyofungwa siku hiyo itajiondokea na kitita kizito cha Pauni milioni 24.4. Ni tofauti Ufaransa waliopokea Pauni milioni 22.1 msimu uliopita.

Haijaishia hapo. Timu itakayoshika nafasi ya tatu itajinyakulia Pauni milioni 21.4, wakati ya nne itabeba Pauni milioni 19.9.

Timu zilizofika robo fainali, kila moja itakuwa na uhakika wa kuzoa Pauni milioni 14, huku kila itakayofika hatua ya 16 Bora ikiwa na Pauni milioni 11.1.

Hatua ya 32 Bora nayo ina zawadi nono ya Pauni milioni 8.1 kwa kila timu, kama ilivyo Pauni milioni 6.6 kwa timu zote zilizoko hatua ya makundi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

spot_img

Related articles

RAIS WA TAIWAN ASITISHA ZIARA YAKE AFRIKA, CHINA IKITAJWA KUWA CHANZO

TAIPEI, TaiwanRAIS wa Taiwan, Lai Ching-te, ameahirisha ziara yake nchini Eswatini, huku akiitaja China kuwa ndiyo chanzo cha...

USIYOYAJUA KUHUSU ZIARA YA PAPA LEO BARANI AFRIKA

KIONGOZI wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Leo XIV, yuko barani Afrika kwa ziara ya siku 10 katika mataifa...

MATESO WANAYOPITIA WATOTO KATIKA MACHAFUKO YA SUDAN

DARFUR, Sudan "HALI ya watoto nchini Sudan inazidi kuwa mbaya kila baada ya saa moja." Hiyo ni kauli ya...

IRAN: TUKO TAYARI KWA VITA MAZUNGUMZO YAKISHINDIKANA

TEHRAN, IranSPIKA wa Bunge la Iran, Mohammad Bagher Ghalibaf, amesema nchi yake itakuwa tayari kwa mbinu mpya za...