KWANINI IRAN IMEGOMA KUACHA MPANGO WA NYUKLIA?

Date:

Share post:

TEHRAN, Iran
KUGOMA kuachana na programu ya nyuklia kumetajwa kuwa sababu kuu ya Iran kushindwa kufikia mwafaka na Marekani katika mazungumzo ya amani ya hivi karibuni mjini Islamabad, Pakistan.

Makamu wa Rais wa Marekani, JD Vance, alisema Taifa hilo linataka kuiona Iran ikikubali kuachana na uzalishaji wa silaha za nyuklia.

Kwa mujibu wake, endapo Iran itakubali, basi Marekani itakuwa tayari kuisaidia katika nyanja zote, ikiwamo kiuchumi.

Kwa miongo zaidi ya miwili, uzalishaji wa nyuklia umetibua uhusiano wa Iran na mataifa ya Magharibi, achilia mbali Marekani.

Kwamba ndiyo chanzo pia cha Marekani kwa kushirikiana na Israel, zilianzisha mashambulizi dhidi ya Taifa hilo Februari 28, 2026.

Kwa mujibu wa Iran, uzalishaji wa nyuklia haulengi kutengeneza silaha, bali kwa matumizi mengine, ikiwamo kuzalisha nishati ya umeme.

Hata hivyo, takwimu zinaonesha tofauti. Kinu cha nyuklia tegemeo cha Bushehr kilichoanza kazi mwaka 2013, kinatoa megawatt 1,000, sawa na asilimia 1 tu ya uzalishaji wa umeme nchini Iran.

Ikimaanisha, asilimia kubwa ya uzalishaji wa umeme nchini humo hautegemei nyuklia, bali gesi asilia na mafuta.

Mtaalamu wa Nishati kutoka Chuo Kikuu cha George Mason, Umud Shokri, anasema: “Iran ndiyo inayoongoza duniani kwa akiba ya gesi asilia na mafuta, hivyo ni gharama nafuu zaidi kuzalisha umeme kwa kutumia vyanzo hivyo kuliko nyuklia.”

Shokri pia anahoji iweje Iran iseme inatumia nyuklia kwa uzalishaji wa umeme wakati bado kiwango kikubwa cha nishati hiyo kinatokana na gesi asilia na mafuta?

“Kwa uhalisia, uzalishaji wa umeme wao unatokana zaidi na gesi asilia. Ni kiwango kidogo sana cha umeme kinachozalishwa kwa nyuklia,” anasema Shokri.

Taarifa zinaeleza kuwa ili Iran itegemee nyuklia kwa uzalishaji wa umeme, kama ambavyo imekuwa ikidai, zinahitajika megawatt 25,000 zaidi.

Kwamba vijengwe vinu vingine 25 vyenye hadhi sawa na kile cha Bushehr, ambacho ujenzi wake ulichukua miaka 20 na kugharimu Dola za Marekani bilioni 11.

Aidha, ripoti za kitaalamu zinaeleza kuwa ututubishaji wa madini ya urani (uranium) kwa matumizi ya binadamu, ikiwamo kuzalisha umeme, unapaswa kuwa kwa asilimia 3-5 tu.

Lakini, Iran imekuwa ikiripotiwa kurutubisha madini hayo kwa asilimia hadi 60, kiwango ambacho hakiwezekani kwa nchi isiyo na silaha za nyuklia.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

spot_img

Related articles

VIONGOZI LONGIDO WATAKIWA KUHARAKISHA UANZISHAJI WA JUHIZINA

Viongozi wa vijiji katika Halmashauri ya Wilaya ya Longido wametakiwa kuongeza kasi ya utekelezaji wa mchakato wa kuanzisha...

LIGI YA EUROPA KUMEKUCHA NUSU FAINALI

LONDON, UingerezaMECHI za marudiano hatua ya robo fainali ya msimu huu wa Ligi ya Europa zilimalizika usiku wa...

MAZUNGUMZO YA ISRAEL, LEBANON KUITULIZA HEZBOLLAH?

BEIRUT, LebanonRAIS wa Marekani, Donald Trump, ameutangazia ulimwengu kuwa viongozi wa Israel na Lebanon wameifikia makubaliano ya kusitisha...

MTANDA AKUTANA NA UONGOZI NA JMAT, KUWAASA USHIRIKIANO NA AMANI

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe. Said Mtanda, amekutana na kufanya mazungumzo na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maridhiano...